Tuesday, 25 March 2014

Huduma bora siri ya tuzo za LAPF

HAPA nchini kuna mifuko mingi ya hifadhi za jamii iliyo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA).Mifuko hiyo imetakiwa na SSRA kukua kwa asilimia saba ili iweze kujiendesha kwa ufasaha na faida kwa wanachama wake.Lakini Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF) umevuka kiwango cha asilimia saba na kufikia asilimia 12, jambo ambalo limewafanya kuweza kupewa tuzo mbalimbali mara tano mfululizo.Tuzo waliyopewa LAPF hivi karibuni ilikabidhiwa  na Rais Jakaya Kikwete ambayo  iliandaliwa na SSRA; na hafla hiyo kufanyika mjini Dodoma katika Bustani ya Nyerere Square.Hata hivyo kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo LAPF walikabidhiwa tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya kupata hesabu bora katika sekta ya hifadhi ya jamii.Hapa Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa LAPF, Valerian Mablangeti anaeleza sababu  za kutwaa tuzo hizo.Anasma  miongoni mwa sababu hizo ni  ongezeko la wanachama lililotokana na uhuru wa kisekta.Anaeleza awali mfuko huo ulikuwa ukiruhusu watumishi wa serikali za mitaa tu lakini sasa umekuwa ukiruhusu wafanyakazi mbalimbali na hiyo ni kutokana na kubadilishwa kuwa wa pensheni.Hata hivyo anasema kanuni bora ya ulipaji wa wanachama na huduma bora inayotolewa kwa wanachama na mfuko huo husababisha mfuko kukua.Mablangeti anasemamwaka 2007/8 mfuko ulikuwa na wanachama 63,302; mwaka  2008/9 walikuwa  69,394; mwaka 2009/10  walikuwa 73,833; mwaka  2010/11  walikuwa 80,529; mwaka 2011/12  walikuwa  91,595 na mwaka 2012/13 matarajio yao yalikuwa ni wanachama 107,000.“Lakini  kuna vitu vingi vinavyochangia kukua kwa mfuko huo, moja wapo ikiwa ni kukua kwa kasi ya rasilimali fedha inayochangiwa na wanachama,” anasema Mablangeti.Historia ya akibaAnasema mwaka 2007/8 mfuko ulikuwa na fedha sh bilioni 179.2; mwaka 2008/9 sh bilioni 271.5;  mwaka 2009/10 sh bilioni 362 na mwaka 2010/11ulikuwa na sh bilioni 450.2.Mablangeti anasema mwaka 2011/12 kulikuwa na akiba ya sh bilioni 539.4 na kwa mwaka 2012/13 mfuko ulitarajia kukusanya sh bilioni 645.Mkurugenzi huyo pia anazungumzia suala la uwekezaji ambapo anasema kama ilivyo kwa taasisi nyingine za hifadhi ya jamii, mfuko unawekeza kwenye maeneo salama, yenye kuleta mapato makubwa .Anasema wanatumia utaratibu ambao wakati wote mfuko unakuwa na fedha za kutosha kulipia mafao ya wanachama ikiwa ni pamoja na maeneo yenye amana za benki, dhamana za serikali, rasilimali za majengo, dhamana za kampuni na hisa za kampuni.“Mfuko umepata mafanikio makubwa katika uwekezaji ambapo hadi kufikia Juni 2011 uwekezaji wa mfuko ulikuwa katika maeneo mbalimbali yote yakiwa na faida kubwa,” anasema Mablangeti.Anasema kulikuwa na amana za serikali na hati fungani kwa asilimia 51, amana za benki asilimia 18, hisa za kampuni asilimia 6, rasilimali za majengo asilimia 11 na mikopo asilimia 14.0.MiradiAnasema mfuko huo umekuwa na ubunifu mkubwa wa miradi mbalimbali ambayo ni pamoja na ya majengo ambayo mfuko unashiriki kuyaendeleza.Anayataja  majengo hayo kuwa ni pamoja na Chuo cha Serikali za Mitaa kilichopo Hombolo, Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Dodoma; Soko la kisasa ‘Shopping mall’ la Mwanza, awamu ya pili ya jengo la ‘Millenium Towers’ la Dar es Salaam, kituo cha mabasi Msamvu, Morogoro, ujenzi wa jengo la makao makuu ya mfuko Dodoma na kituo cha malori Mbezi Louis.Mkurugenzi huyo anaelezea ulipaji wa mafao kwa kusema kwa mujibu wa sheria Na. 9 ya mwaka 2006 walitekeleza ulipaji wa mafao mbalimbali ulioanza Januari 2007.Anaainisha mafao hayo ni ya uzeeni, mirathi, ulemavu, uzazi, msaada wa mazishi na mafao ya kujitoa kazini.Anasema kuanzia mwaka 2007 hadi Juni 2011, wastaafu 4,969 wamelipwa jumla ya sh bilioni 73.2  ikiwa ni stahili za mafao yao.Anasema moja ya mikakati ya mfuko ni kuhakikisha ustawi wa wanachama unaendelea kuboreshwa na katika kutekeleza hilo, mfuko umeanzisha huduma nyingine zinazolenga kuwanufaisha wanachama ambazo ni mikopo ya nyumba na mikopo kupitia Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) vya wanachama.Mikopo ya nyumbaAkizungumzia kuhusu mikopo ya nyumba, anasema wameanzisha utaratibu wa kuwakopesha wanachama sehemu ya mafao yao kwa ajili ya ujenzi wa nyumba pale wanapokaribia kustaafu hususan wanapofikia miaka 55.Anasema kiasi cha mkopo kinachotolewa ni nusu ya mafao ya mkupuo ambayo yangetolewa endapo mwanachama angestaafu.“Mpango huu umewasaidia sana wanachama wengi kumiliki nyumba zao wenyewe kabla ya kustaafu ambapo hadi kufikia Juni  2011 jumla ya wanachama 52 walipata mikopo ya sh bilioni 1.07,” anasema Mablangeti.Mikopo ya SaccosKatika kipindi cha mwaka 2008/09 walianzisha huduma ya mikopo kwa wanachama wote kupitia vyama vyao vya Saccos katika maeneo yao ya kazi.Anasema Saccos zilizofanikiwa kupata mikopo ni kutoka Njombe, Kilombero, Songea na Igunga ambapo  sh bilioni moja zilikopeshwa kwa wanachama hao tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo.Lakini anasema kila palipo na mafanikio hapakosi changamoto ambazo anazitaja kuwa ni pamoja na ushindani unaotokana na uhuru wa watumishi wapya kuchagua mfuko wa kujiunga, makao makuu ya mfuko kuendelea kuwa Dodoma, maeneo ya uwekezaji kuwa finyu, pamoja na waajiri kutowasilisha michango kwa wakati.Changamoto nyingine ni pamoja na  mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha lakini anaahidi kuwa mfuko utaendelea kujipanga ili kuhakikisha kuwa changamoto hizo hazileti athari katika uendelevu wake.inShare

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: