Thursday, 25 August 2016

Wednesday, 24 August 2016

Tuesday, 23 August 2016

Mpiga tarumbeta wa Bob Marley, afariki

Mpiga tarumbeta Headley Bennett, ambaye alishiriki katika wimbo wa kwanza wa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za rege Bob Marley 'Judge Not,' amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Mwanawe Carol Bennett, alithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo siku ya Jumapili.
Carol hakusema sababu maalum ya kifo cha mwanamuziki huyo, lakini alisema babake alikuwa akiugua shinikizo la damu na hivi majusi alipatika na saratani ya kiume.
Bennett alishiriki kwa muziki wa Gregory Isaacs na Jimmy Cliff
Benneth alishiriki na wanamuziki wa nyimbo za rege kama vile Bunny Wailer na Gregory Isaacs.
Alituzwa na serikali ya Jamaica mwaka wa 2005 kama Mjamaica wa sita mwenye hadhi ya juu.
Alichokiandika Raymond wa WCB baada ya kupewa zawadi ya gari


Moja ya headline kwenye mitandao ya kijamii iliyochukua nafasi usiku wa August 22 2016 ni pamoja na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa staa wa bongo flava kutokea katika label ya WCB Raymond ambapo uongozi wake uliamua kumfanyia suprise ya zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4 yenye thamani ya milioni 20 za kitanzania.
Leo August 23 Raymond kupitia ukurasa wake wa instagram aliamua kuyatoa yake ya moyoni kwa kuandika…>>>’Kweli Nimeamini Mungu Hana upendeleo.nilikua mtu nilie jikatia tamaa ndani ya miaka takribani mi nne nilikua nikiangaika na muziki wangu nakushukuru sana sana
‘Kaka Lao Diamond Platnumz Umenifundisha vitu vingi saaaaaanaaa hadi leo naiona njia boss wangu Babu Tale ni mwaka wa tano sasa toka Umenijua umenivumilia kwa mengi hadi leo hii haujanichoka na unanisaidia kwa moyo mmoja’
Boss Sallam Sk Asante sana kwakupigania kila siku thamani ya muziki wangu nakuakikisha nafika sehemu nzuri Mkubwa Fella wewe ni zaidi ya mzazi maana umenilea nakunifundisha meeengi kwenye muziki
‘Madee Sitoacha kukushukuru kaka lao wewe nikioo naamini unafurahi kuniona mdogo wako hapa nilipo maana unanijua saaaaanaaaa

Monday, 25 July 2016

Thursday, 14 July 2016

Nyimbo kumi bora zaidi kwa harusi duniani

Wimbo wa mapenzi wa mwanamuziki wa Uingereza Ed Sheeran unaongoza kwa kupendwa sana na watu kama wimbo wa kufungua jukwaa wakati wa harusi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Spotify, ambao wamechunguza maelfu ya orodha ya nyimbo zinazosambazwa zaidi katika mtandao huo, wimbo wa Thinking Out Loud unaongoza.
Wimbo wa At Last wake Etta James ni wa pili nao wimbo wa Ray LaMontagne, You Are the Best Thing ni wa tatu.
Nyimbo nyingine maarufu zilizo kwenye orodha ya 50 bora duniani ni wimbo wake Frank Sinatra uitwao The Way You Look Tonight na wimbo wa Marry You wake Bruno Mars.
Nyimbo kumi zinazopendwa zaidi duniani kwa mujibu wa Spotify, mtandao unaowawezesha watu kusikiliza nyimbo moja kwa moja mtandaoni, ni:
  1. Thinking Out Loud - Ed Sheeran
  2. At Last - Etta James
  3. You Are the Best Thing - Ray LaMontagne
  4. All of Me - John Legend
  5. A Thousand Years - Christina Perri
  6. Make You Feel My Love - Adele
  7. I Won’t Give Up - Jason Mraz
  8. Everything - Michael Bublé
  9. Better Together - Jack Johnson
  10. Amazed - Lonestar
Polisi watinga Nyumbani kwa Diamond na Kuzima Sherehe, Kisa?




Taarifa kutoka katika Magazeti ya Udaku na Blogs kadhaa mjini zinaeleza kuwa Polisi wenye Silaha hivi karibuni walifika Nyumbani kwa msanii Diamond Plutnumz na kuzima Shughuli iliyokuwa ikiendelea.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, shughuli iliyositishwa  na polisi ilikuwa ni ile ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa mkali huyo wa muziki, Sanura Kassim ‘Sandra’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Ilidaiwa kwamba msanii huyo amekuwa akifanya sherehe mara kwa mara katika nyumba yake hiyo, hali inayosababisha kero kwa baadhi ya majirani zake, ambao nao, wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwa viongozi wa serikali ya mtaa huo.
dc49DIAMOND11
Gazeti hili baada ya kuupata ubuyu huo, lilifunga safari hadi nyumbani kwa msanii huyo na ku kia ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha ambaye baada ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa tukio hilo la askari kuzima sherehe hiyo, alikiri kuwa ni kweli.
“Nimekuwa nikipata malalamiko ya mara kwa mara kuhusu sherehe za Diamond kuwa waalikwa wake ni vijana wa kihuni ambao wakija huwa wanavuta bangi hadharani, wanafunga barabara pamoja na kujisaidia haja ndogo hovyohovyo maeneo ya nje ya nyumba yake.
mwenyekiti 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha.
“Juzi nilipigiwa simu usiku na majirani zaidi ya sita wakila lamika kuhusu sauti kubwa ya muziki wa kwenye sherehe ya Diamond, nilimuita lakini akakaidi, ikabidi niende Kituo cha Polisi cha Wazo na kuchukua polisi wakiwa na silaha na kwenda kufunga sherehe ile, sheria iko wazi kuhusu utaratibu wa kupiga muziki maeneo ya baa na majumbani,” alisema Kamugisha.
Baadhi ya majirani waliozungumza na gazeti hili, walisema kumekuwa na tabia ya Diamond kufanya sherehe mara kwa mara nyumbani hapo, huku muziki mkubwa ukipigwa, jambo ambalo kwao ni kero.
“Nachukizwa sana na kelele za Diamond, kwani watu tunashindwa kulala kwa sababu yeye anafanya sherehe mbona kuna kumbi na hoteli anaweza kwenda tu, mimi nyumba yangu ni kama kilomita mbili kutoka kwake, lakini nasikia muziki kwa kero, je walio ubavuni mwake si wanataabika sana!” alisema mzee mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Gazeti hili lilimtafuta Diamond kwa simu yake mkononi ili kuzungumzia ishu hiyo lakini iliita bila kupokelewa kwa muda wote.

Wednesday, 13 July 2016

VIDEO ,AKOTHEE SONG YUPO MOYONI
Akothee ni msanii wa kwanza wa Kenya kufanya kolabo na mwimbaji Mtanzania Diamond Platnumz kwenye ile single yake iitwayo Sweet Love, sasa time hii ametuletea hii video mpya ya single yake iitwayo Yuko moyoni.

Thursday, 30 June 2016

Monday, 9 May 2016

Tuesday, 3 May 2016

SAD NEWS..!! Mama mzazi wa Tupac Shakur afariki dunia akiwa na miaka 69.

 SAD NEWS..!! Afeni Shakur Davis,mama mzazi wa the late Tupac Shakur amefariki dunia akiwa na miaka 69,kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Sausalto,California wamedai kuwa Afeni alifariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwahishwa hospitali mara baada ya kupata taarifa ya simu ya dharura kutoka nyumbani kwake.
Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi inayoeleza chanzo cha kifo chake,so lets wait and see.Tupac Shakur's Mother Afeni Shakur Davis Dies at 69: Police
                                                             Afeni Shakur.
Tupac ambae ni miongoni mwa rappers wanaoheshimika na jamii ya wanamuziki wa HipHop Ulimwenguni alipigwa risasi September 7 1996 jijini Las Vegas,Nevada na kufariki baada ya siku 6 akiwa na umri wa miaka 25.
PACCCCCCCCCCCCCCCCCCCCCSSSSSS                                                          Hayati Tupac Shakur.
PICHA YA ZARI NA IVAN YAZUA UTATA HUKO INSTAGRAM

Huku Instagram picha hizo mbili zimekuwa gumzo leo baada ya Mama mtoto wa Diamond kwasasa Zari Hassan na aliyekuwa mumewe Ivan Kuonekana wamepiga picha sehemu moja inayofanana kwenye sehemu ya kuogelea. 

Picha hizi zimeleta wasiwasi kuwa huenda wawili hao walikuwa pamoja wakiogelea huku wengine wakimtetea Zari na kusema kuwa yeye alikuwa hiyo sehemu...
siku nyingi lakini Ivan ameenda sehemu hiyo hiyo na kupiga picha na kuzitupia mtandaoni leo kumuumiza Diamod na kuwapa watu cha kuongea.
Kesi ya Kitilya na wenzake Leo May 03 2016 haya hapa maamuzi ya Mahakama

Kesi ya Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni Miss Tanzania 1996, Shose Sinare.
images-Miss_696029087
Kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa leo May 3 2016 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo imehailishwa tena hadi Mei 18 2016 kutokana na Jalada la kesi hiyo ambalo lilitegemewa kurudi leo lakini halijarudi na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande.
Aidha watuhumiwa walitakiwa kufika mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea na rufani ambapo baada ya kufika Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kuanza kusikiliza rufani hiyo May 5 2016.
Mikoani walikuwa hawaamini kama sisi ndio tuliyoimba wimbo ‘Kamatia Chini’- Aika
Msanii wa kundi la Navy Kenzo, Aika, amefunguka na kuzungumzia faida ya tour yao ya ‘Kamatia Chini Tour’ ambayo ilifanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Navy Kenzo
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Aika amesema tour hiyo iliwasaidia kuwatangaza kwani walikutana na mashabiki wao ambao walikuwa hawaamini kama wao ndio wameimbi wimbo ‘Kamatia Chini’.
“Kuna vitu vingi kama wasanii tumejifunza, next time ili tujirekebishe na kusawazisha makosa yetu na kufanya kitu kikubwa zaidi,” alisema Aika.
“Mapokezi ya ‘Kamatia Chini’ mkoani yalikuwa makubwa sana isitoshe wimbo ulikuwa hata haijafikisha wiki 2, lakini kila mtu alikuwa anaimba, yaani watu walivyosikia wale watu waliyoimba ‘Kamatia Chini’ wamefika, wengine walikuwa wanakataa. Wanasema hawawezi kuwa hawa, lakini sisi tukawaonyesha sisi ni Watanzania na ndiye tuliyoimba ule wimbo,” aliongeza Aika.

Monday, 2 May 2016

Sunday, 1 May 2016

Upande wa pili wa mkasa wa ndoa ya Tiwa Savage utakuacha mdomo wazi
Mume wa Tiwa Savage, Tee Billz alipost mfululizo wa malalamiko kwenye Instagram kuhusu kumtuhumu mke wake kuwa alimsaliti na Doj Jazzy, Dr Sid na 2Face Idibia.
Tiwa-Savage-Traditional-Wedding-Tee-Billz-TJ-Balogun-BellaNaija1-142
Jamaa huyo alionesha nia ya kutaka kujiua kutokana na masahibu hayo. Hiyo ilipelekea jamii kubwa ya Nigeria imchukie Tiwa kwa kumuona kama mwanamke katili na anayemtesa mumewe. Lakini upande wa pili wa shilingi wa mkasa huo unaweza ukabadili mawazo yako.
Kwa mujibu wa Tiwa, mume wake ndiye mzinguaji mkubwa na ana vimbwanga haswaa.
Akiongea kwenye exclusive interview na Pulse TV, Tiwa alisimulia jinsi ambavyo mume wake alikuwa akimfanyia ikiwa pamoja na kumtelekeza kwa kutotaka kujua chochote pale alipolazwa hospitali nchini Jamaica alikoenda kufanya video na Busy Signal.
Anasema wakati anajiandaa kwenda kushoot, alianza kutoka damu nyingi ukeni kiasi cha kupoteza fahamu. Alimpigia simu na kumtumia ujumbe mumewe ikiwa pamoja na kumtumia picha akiwa hoi kitandani lakini hakujibiwa hadi anatoka hospitali.
Siku amerejea Nigeria na akiwa amelala usiku wa saa nane, simu ya mumewe iliita kwa namba iliyohifadhiwa kwa jina la biashara lakini alishangaa iweje kampuni impigie usiku huo. Anadai alichukua simu ya mumewe na kuanza kusoma ujumbe wa WhatsApp na ndipo alipogundua kuwa huyo alikuwa ni mwanamke na maongezi yao yalionesha kuwa walikutana hotelini na kufanya mapenzi. Kutokana na kitendo hicho aliondoka na kwenda kwa rafiki yake.
Anadai kuwa amekuwa akificha kwa muda mrefu kuhusu mume wake, lakini amedai tangu mtoto wao azaliwa, hajawahi kutumia hata senti kwaajili ya familia yao kwamba Tiwa ndiye kila kitu.
Amesimulia pia jinsi ambavyo mume wake amekuwa na tabia ya kumzunguka kwenye malipo ya show zake ambapo ametolea mfano wa harusi aliyotakiwa kwenda kutumbuiza London. Anasema alibaini kuwa mumewe alilipwa gharama zote lakini hadi anaenda kutumbuiza alimueleza kuwa hakuwa amelipwa. Kwakuwa alikuwa anafahamiana na miongoni mwa waandaji wa harusi hiyo alimuuliza na kujibiwa kuwa walikuwa wameshamlipa mume wake hela yote, miezi minne nyuma.
“Unamuibia mke wako, na yeye haoni kama ameniibia mimi, kwahiyo ilibidi nitumbuize kwenye harusi bure, kwasababu alikuwa ameshatapeli hela na sijui alizifanyia nini,” anasimulia.
Kwa upande mwingine staa huyo alieleza jinsi ambavyo mume wake alikuwa akiishia maisha ya zaidi ya kipato chake na hivyo wakati mwingine kumfanya ajikute kwenye madeni makubwa ambayo alilazimika kuyalipa.
Tiwa anasema jambo ambalo mume wake alizingua zaidi na ambalo limesababisha mgogoro wao ni pale alikopa naira milioni 45 ambazo ni sawa na shilingi milioni 495 za Kitanzania na kuchikichia. Kwa hali hiyo Tiwa alianza kuhofia usalama wake kwamba wanaomdai mumewe wangeweza hata kumdhuru ama kumteka yeye na mwanae kwasababu ya deni hilo.
Pia Tiwa amezungumzia jinsi ambavyo aligundua mume wake anatumia cocaine kitu ambacho kilimuumiza sana.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alikanusha kwa msisitizo kuwa hajawahi kamwe kumsaliti mume wake na Don Jazzy, Dr Sid wala 2Face na kwamba yupo tayari hata kuwekewa kifaa cha kubaini kama anasema uongo.
Mpaka hapo Tiwa ameonesha nia ya kuachana na mume wake, kitu ambacho anadai hakupenda kiwe.
Video: Joti aja na vituko hivi Youtube

Wasanii wa vichekesho nchini wameanza kuamka na kutambua kuwa Youtube ni mtandao unaoweza kuwapa mkwanja mzuri kama wakiutumia ipasavyo. Joti ameamua kuja na series za vituko vyake ambavyo anaweka Youtube kwaajili ya kuvunja mbavu mashabiki wake. Check hiyo video ya kwanza.