Msanii wa kundi la Navy Kenzo, Aika, amefunguka na
kuzungumzia faida ya tour yao ya ‘Kamatia Chini Tour’ ambayo ilifanyika
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Aika amesema tour hiyo iliwasaidia
kuwatangaza kwani walikutana na mashabiki wao ambao walikuwa hawaamini
kama wao ndio wameimbi wimbo ‘Kamatia Chini’.
“Kuna vitu vingi kama wasanii tumejifunza, next time ili
tujirekebishe na kusawazisha makosa yetu na kufanya kitu kikubwa zaidi,”
alisema Aika.
“Mapokezi ya ‘Kamatia Chini’ mkoani yalikuwa makubwa sana isitoshe
wimbo ulikuwa hata haijafikisha wiki 2, lakini kila mtu alikuwa anaimba,
yaani watu walivyosikia wale watu waliyoimba ‘Kamatia Chini’ wamefika,
wengine walikuwa wanakataa. Wanasema hawawezi kuwa hawa, lakini sisi
tukawaonyesha sisi ni Watanzania na ndiye tuliyoimba ule wimbo,”
aliongeza Aika.
0 comments: