Thursday, 25 August 2016

Mwanamume  abeba maiti ya mkewe 12km

Amang Majhi alifariki dunia kwa maradhi ya kifua kikuu Jumanne usiku
Mwanamume mmoja maskini nchini India alibebe maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alimofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.
Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.
Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.
Hospitali hiyo imekana madai hayo.

'Hakuna namna'

'Mwanamke huyo alilazwa hospitalini siku ya Jumanne na kufariki usiku huo huo.
Bwana yake alichukua maiti hiyo bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,' afisa mkuu wa afya B Brahma alisema
Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Juma nne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumsihi kuondoa mwili huo.
' Nilikuwa nikiwaomba wahudumu wa hospitali hiyo wanisaidie gari nimbebe mke wangu lakini nikaambulia patupu.
Kwa sababu mimi ni maskini na nisingeweza kukodisha gari la kibinafsi sikuwa na njia nyingine ila kumbeba mke wangu mabegani.'

Wakati akitembea , Bw Majhi alisindikizwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 12 , Chaula
Mapema Jumatano , alisema alifunga mwili wa mkewe na nguo na kuanza safari hiyo ndefu ya kuelekea kijijini huko Melghar kwa mila na tamanduni za mwisho akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12 , Chaula.
Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake.
Shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku

Thursday, 14 July 2016

Shambulio laua watu zaidi ya 80 Ufaransa

Zaidi ya watu 80 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa.
Lori lililokuwa likienda mwendo kasi lilijiingiza katika mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiangalia maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille, ambayo huja na shamra shamra kila mwaka.
Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre amesema lori hilo liliendelea kutembea kilo mita mbili kabla ya polisi kumpiga risasi dereva.

Rais Francois Hollande amerudi mjini Paris kwa ajili ya kufanya kikao cha dharura.
Hali ya tahadhari iliyowekwa toka kutokea kwa shambulio lililofanywa na Islamic State mjini Paris, bado iko palepale nchini Ufaransa.
Huyu ndiye Kuku Ghari zaidi Duniani, Jogoo anauzwa kwa Dola 2000 za Kimarekani.


Basi unaambiwa kuwa hii ndiyo aina ya Kuku mwenye gharama kubwa zaidi Duniani.. Ukihitaji Jogoo mmojawapo aliyekomaa ili umfuge basi itabidi uwe na $2000., Na sababu kuwa ni kwa sababu wapo wachache mno.
Kuku hawa wanafahamika kama ‘Ayam Cemani’ chimbuko lao ni kule Indonesia, unaambiwa kila kitu kwenye Mwili wao ni cheusi, kuanzia ngozi, maini, utumbo, macho, moyo, ubongo, kiini cha yai lake, nyama yenyewe mpaka kinyesi chao…
Sababu ya weusi huu ni kutokana na wingi wa Melanin kwenye seli zao na hali hii kijenetiki hufahamika “fibromelanosis”.
Raia wa Uganda waweka picha za utani mitandaoni baada ya Rais Museveni kuongea na simu pembeni ya barabara

Jana Julai 12 Rais wa Uganda, Yoweri Museveni alisimamisha msafara wake na kuketi pembezoni mwa barabara ambapo alizungumza na simu kwa takribani dakika 30.
Baada ya raia wa nchi hiyo kuona kitendo hicho, nao walianza kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wanaongea na simu pembezoni mwa barabara na wengine ku-edit picha ya Rais Museveni na kuiweka maeneo tofauti tofauti
Hapa chini ni picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii.
- -- --- ---- ----- ------ ------- -------- 1 (1) 2 (1) 2 (2) 11 12 13 14 15 16

M72 M73 M74 m76

Wednesday, 13 July 2016

Unyonyaji kidole unafaida kwa watoto- Utafiti
Ripoti mpya inasema watoto wanaonyonya vidole au kung'ata kucha zao kwa meno huenda wasipate matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.
Kwa mujibu wa waandishi katika jarida la Pediatrics, huo ni ni usafi dhanio,kwani yatokanayo na baadhi ya wadudu huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
Unyonyaji wa kidole gumba na ung’ataji wa kucha umeonekana kuzuia baadhi ya alergy.
Kati ya watu elfu moja wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi thelathini na mbili,walifanyiwa uchunguzi kwa muda nchini New Zealand.
Lakini tabia hii ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali.
Uchunguzi uliofanywa na kurekodiwa kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka mitano na kumi na moja na wengine waliofanyiwa vipimo ni wenye umri kati ya miaka kumi na tatu na thelathini na miwili.
Huku thuluthi moja ya watoto hao ni wanyonyaji wa vidole mara kwa mara au hung’ata kucha zao na katika vipimo walivyofanyiwa watoto hao wameonekana kuwa wana kiwango kidogo cha kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.

Watoto wanaoweza kupata matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani (alergy) kutokana na vitu kama vumbi kutoka majumbani,manyoya ya paka au mbwa, lakini watoto wenye kunyonya vidole gumba na kung’ata kucha walikuwa ni chini ya theluthi moja kuliko watoto wenye tabia hii ya unyonywaji vidole.
Na tabia hii ya unyonyaji vidole au ung’ataji kucha inaonekana kuwa kinga mpaka wanapofikia umri wa utu uzima.
" kuwa na paka au mbwa majumbani,ndugu au jamaa wanaofanya kazi mashambani pia imeonekana kuwa ni sababu kubwa inayosababisha mazingira ya ukuaji wa magonjwa yanayosababishwa na
kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.

Thursday, 21 April 2016

Director wa filamu za James Bond afariki akiwa na umri wa miaka 93


Muongazaji wa filamu ya James Bond Guy Hamilton amefariki akiwa na umri wa miaka 93.
Aliyekuwa nyota wa filamu hiyo ya 007 Roger Moore alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba alihuzunishwa na kifo chake.
160421152808__guy_hamilton_640x360_afp_nocredit
Guy Hamilton
Hamilton alimuelekeza Roger Moore katika filamu ya Live and Let Die pamoja na The man with the Golden Gun.
Pia alifanya uelekezaji katika filamu za Sean Connery in GoldFinger na Diamond are Forever.
1606
Hospitali moja katika kisiwa cha Uhispania cha Majorca ,ambapo Hamilton aliishi ilithibitisha kwa chombo cha habari cha AP kwamba amefariki sikju ya Jumatano.
Filamu nyengine zilizoelekezwa na Hamilton ni pamoja na The Battle in Britain,Force 10 from Navarone,Evil under the sun na The Mirror Crack’d.
Source: BBC & theguardian
Kijana akatwa mkono wakati akijaribu kuiba simu kupitia dirishani

post-feature-image


Mmiliki wa simu hiyo akiwa ndani aliona mkono wa mtu ukitumbukia nakupapasa simu kupitia dirishani, ndipo alipoamuwahi kwa kumkata mkono kwa panga

Kijana mmoja huko Nigeria katika mji wa Delta State, amejikuta akipoteza mkono wake kwa kukwatwa na panga wakati akiwa kwenye harakati za kuiba simu kupitia dirishani.

Kwamujibu wa King Tino, tukio hilo lilitokea usiku wakuamkia leo eneo liitwalo Sepele. Mmiliki wa simu hiyo akiwa ndani aliona mkono wa mtu ukitumbukia nakupapasa simu kupitia dirishani, ndipo alipoamuwahi kwa kumkata mkono kwa panga.

Kijana huyo aliamua kutimua mbio huku akipiga ukunga nakuacha mkono wake ukiwa ndani ya chumba umekatwa. Lakini alikamatwa mapema nakuwahishwa hospitalini.

Friday, 15 April 2016

JASIRI ALIYESHINDWA KUKABILI CHANGAMOTO ZA NDOA





Na Zuhura Simba

Mwanasiasa Mkongwe na Mwanaharakati aliyepambana na sera za ubaguzi za makaburu wa Afrika Kusini na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mwafrika nchini humo. Ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel. Pia amepata kutunukiwa zaidi ya tuzo 250 katika miongo minne iliyopita.

Ni Rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa Chama cha African National Congress (ANC) aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Pamoja na ushujaa huo wa Nelson Mandela,katika Maisha yake ya Ndoa alipata changamoto nyingi sana ambazo alijitahidi kuzikabili bila mafanikio.

Wengi tunajua jinsi ndoa ilivyo na changamoto kubwa. Wengine wana mawazo kwamba Mungu, hakupanga taasisi hii (ndoa) iwe ilivyo sasa, ya mme mmoja na mke mmoja au hata kufunga ndoa; kwamba alituumba tuishi kama wanyama! Bila kuwa na kifungo cha ndoa!

Haya yanasemwa baada ya ndoa nyingi kukumbwa na changamoto. Mahatma Gandhi, alifikia hatua ya kutaka kuishi na mke wake, kama mtu na dada yake.

Walifanya kiapo cha kuacha uhusiano wa kimwili – uhusiano wa ndoa, ili waishi kama ndugu. Alikuwa tofauti na Mandela kwani yeye hakuvunja ndoa yake bali aliishi na mkewe kama mtu na dada yake.

Hali ilikuwa tofauti kidogo kwa upande wa Nelson Mandela kwa kutoweza kuishi na Winnie kama mtu na dada yake hii ndo imepelekea leo hii awe ni shujaa lakini alishindwa kustahimili changamoto za ndoa. .

Hakuna asiyejua ni jinsi gani Madiba alivyoshinda mitihani mingi kwenye maisha yake lakini kama ilivyo ada hakuna mkamilifu kwenye dunia hii.

Pamoja na heshima zote tunazompatia Mzee Mandela, alibaki ni mwanamume wa kiafrika mwenye kuutukuza mfumo dume.

Katika vitabu vya historia ya Mandela,kuna baadhi ya vitabu vilivyomuonesha akimfanyia unyanyasaji wa kijinsia mkwewe wa kwanza Evelyn,kiasi cha kuwaleta wapenzi wengine kwenye kitanda chao cha ndoa na kumlazimisha Evelyn kulala uvunguni mwa kitanda.

Pia Mzee Mandela, hakutaka Winnie afanye kazi yoyote, alimtaka akae nyumbani na kuwalea watoto. Ukisoma barua ambazo Mandela alikuwa akimwandikia Winnie, kipindi ambacho alikuwa gerezani utaona alivyokuwa akisisitiza kuwa mkewe akae nyumbani ili alee watoto na yeye ndo atakeyehakikisha mahitaji yote kama kichwa cha familia.

Hii hali haikuwa kwa Winnie peke yake hata kwa mke wake wa kwanza Evelyn naye alipata changamoto ya kutekeleza mapenzi ya Mandela kwa jinsi atavyotaka Mandela kama mume na baba mwenye nyumba.

Evelyn,alikuwa Mkristu mwenye itikadi kali,ilikuwa vigumu sana kukubali kuchanganya suala la siasa na hakukubali kuchanganya dini na siasa. Na hakukubali kutekeleza mapenzi ya baba mwenye  nyumba. Hata hivyo, kinyume cha ndoa ya Winnie, kwa Evelyn, aliyeshinikiza ndoa hiyo kuvunjika si Mandela.

Evelyn mwenyewe ndiye aliweka masharti ya ama Mandela kumchagua yeye au kuichagua siasa na Mandela, akaamua kuichangua siasa na ndoa yao ikavunjika.

Mbali na tatizo hili la mfumo dume la mwanamke kutekeleza mapenzi ya baba mwenye nyumba, mfumo ambao umezivuruga ndoa nyingi za kiafrika au kusababisha wanawake wengi wa kiafrika kuishi maisha magumu kwenye ndoa zao, Mzee Mandela alikuwa na tatizo la kutopata nafasi ya kutosha kusoma na kuelewa tabia za wapenzi wake.

Alikuwa akivutiwa na sura, muda mfupi anatangaza ndoa. Ilitokea kwa Evelyn, ikatokea kwa Winnie na hata kwa mkewe wa mwisho, Graca.

Kwenye kitabu chake cha Long Walk To Freedom, ukurasa wa 101 anasema; “Siku chache baada ya kukutana na Evelyn, kwa mara ya kwanza, niliomba kumtoa. Haraka haraka tulianza mapenzi na miezi michache baadaye niliomba tufunge ndoa, akakubali..”. Pia anaelezea jinsi Evelyn alivyokuwa msichana mzuri na wa kuvutia.”

Na ukurasa wa 214, Mandela anaandika: “Siamini kama kuna mapenzi ya papo kwa hapo, lakini nilipokutana na Winnie Nomzamo, kwa mara ya kwanza, niliamini nataka awe mke wangu..”

Na ndivyo ilivyokuwa, walifunga ndoa na Winnie, muda mfupi baada ya kukutana. Na historia iliyofuata, haikumpatia nafasi Mandela, kumfahamu Winnie. Harakati za kupigania uhuru na hatimaye kifungo cha miaka 27, ulikuwa ukuta mkubwa kati ya Winnie na Mandela.

Baadhi ya vyombo vya habari vilieleza jinsi uhusiano wa Graca Marchel na Mzee Mandela ulivyoanza. Mara ya kwanza alipokutana na mama huyu, Mzee Mandela aliuliza wasaidizi wake “ Huyu Mama mzuri hivi ni nani?”

Wakamjibu ni “Mke wa marehemu Samora Marchel”. Alipokutana na Graca, mara pili, Mzee Mandela, hakukumbuka alishatambulishwa, aliuliza swali lile lile “Huyu Mama mzuri hivi ni nani?” Akajibiwa tena ni “Mke wa Marehemu Samora Marchel”.

Ilipotokea mara ya tatu akaamua kutupa karata ya kufunga ndoa. Yawezekana kwa ndoa hii ya tatu, Mzee Mandela, amepata nafasi ya kuangalia mbali zaidi ya sura. Wake zake wawili wa mwanzo Evelyn na Winnie, alitamani sura zao na kuwataka wayatimize “mapenzi yake”, hakupata nafasi ya kuangalia na kujifunza kwa undani karama zao na kuziachia karama hizo kuchanua.

Mzee Mandela, alivutiwa na sura, lakini hakuwa tayari kuyapokea na yale ya ndani. Evelyn, alipotoa ya ndani, na kuonyesha kwamba yeye si sura tu bali ana  mengine yanayounda “utu”  wake na upekee wa yeye kuitwa ni fulani, Mzee Mandela hakuwa tayari kuyapokea na ndoa yao ikaishia hapo.

Vile vile kwa Winnie, Mzee Mandela alivutiwa na sura yake, lakini hakuwa tayari kupokea yale ya ndani. Winnie, mpambanaji, Winnie mwanasiasa, kwa vile kwa kipindi kirefu hawakuishi pamoja kuweza kufahamu mambo ya ndani ya Winnie, alipotoka gerezani na kupata nafasi ya kumfahamu Winnie alivyo, Mzee Mandela, alishindwa kabisa kumpokea jinsi alivyo. Winnie, mwenye sura nzuri ya kuvutia, alikuwa sasa ni Winnie mwanasiasa na Winnie mpambanaji. Mzee Mandela, akafunga milango ya moyo wake na kuanza mbio nyingine za kumtafuta mwenza mwingine.

Ndoa, ni kuunganisha watu wawili wasiofanana! Watu wawili ambao si ndugu wala jamaa! Ndoa ni    kuunganisha watu wawili wenye tabia tofauti na karama tofauti. Hivyo ukiweka mfumo dume pembeni, ndoa inahitaji uvumilivu wa pande zote mbili, kusameheana kwa pande zote mbili, kuchukuliana kwa pande zote mbili, kila upande ukiziachia karama za upande mwingine kuchanua. Hivyo ikitokea ndoa ikavurugika na kuvunjika, si haki mzigo kubebeshwa upande mmoja.

Inawezekana Winnie, alifanya makosa na labda alitembea nje ya ndoa kama wanavyosema wengine, lakini ukilinganisha na kujitoa kwake kwenye mapambano ya kuleta uhuru wa watu wa Afrika Kusini, kampeni za kufunguliwa Mandela na kuendeleza jina la Mandela, wakati Mandela akiwa gerezani, jinsi naye alivyokamatwa na kufungwa zaidi ya mara 23, uzalendo wake kwa nchi yake, yangefunika makosa yake madogo na hasa kwa mtu kama Mandela, ambaye anatueleza aligundua faida ya kutafakari akiwa gerezani.

MTEMBEZI

Tuesday, 12 April 2016

Baada ya kumtimua Anne Kilango, Rais Magufuli Asema Ametuma Watu Kuwarekodi Mawaziri Wanaolalamika ili nao Awatumbue Majipu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe  Magufuli amesema amewatuma watu kuwarekodi mawaziri ambao wamesikika wakilalamika 'chinichini' kukatwa kwa fedha za matumizi mengineyo ( OC- Other Charges )  katika bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha.

"Mawaziri wengine nasikia wanalalamika kweli,sasa nimetuma watu kuwarekodi kwa sababu mind set (fikra) zao bado hazijabadilika,wanafikiri watu bado tupo kwenye trend  hiyo hiyo,wasomi ni wengi,unaweza ukawateua leo na kesho ukawabadilisha, ili mradi twende kwenye trend ninayoitaka," alisema Magufuli.

Rais Magufuli  aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia hatua ya bunge kubana matumizi na kuwezesha kupatikana kwa kiasi cha shilingi bilioni 6 ambazo zitaelekezwa kwenye utengenezaji wa madawati.

“Chief Secretary(Katibu Mkuu Kiongozi ), huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu, waache kudai OC… Nawasikia watu wanadai eti OC ni kidogo. Wakiona hazitoshi basi waache kazi, maana wenzao wabunge wamesema ni nyingi na wamebana matumizi," alisema Rais Magufuli na kuongeza:

"Katibu wa bunge ameonyesha mfano,kwa nini wengine washindwe? Mtaona katika bajeti tumekata hizo OC ambazo zilikuwa ni ulaji mtupu, tumeongeza bajeti ya maendeleo kutoka kati ya bilioni 26 na 27 hivi za mwaka jana hadi asilimia 40, fedha za bajeti ziende kufanya miradi ya maendeleo, zikawasaidie watu masikini."
Madudu Kibao Yabainika Katika Uhakiki wa Madeni ya Watumishi Wanayoidai Serikali

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) , amefanya uhakiki wa madeni yanayodaiwa serikali na watumishi na kubaini madudu kibao.

Amesema madai mengine yameonyesha mashaka ambapo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wakuu wa ndani kujiridhisha ukweli wa madai hayo kabla ya kuyafikisha serikalini kwa ajili ya malipo.

“Madai mengine yanatia mashaka, sisi hatuhitaji kuletewa madeni ya hovyo hovyo ni vema Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wa ndani wakajiridhisha kabla kuyapeleka serikalini kwa ajili ya malipo.

"Madeni mengine ya ajabu, mfano unakuta mtumishi mmoja anaidai serikali sh. milioni 30,  jambo ambalo ni gumu hata kama alihamishwa haiwezekani kufikia kiwango hicho, pia kuna baadhi ya majina yamejirudia mara nne,” amesema.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa alipotembelea Hospitali hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kukabidhi msaada wa vifaa tiba alivyovitoa kwa ajili ya hospitali hiyo.

Amesema kuwa serikali italipa madeni yote inayodaiwa baada ya kumaliza kuyafanyia uhakiki, hivyo aliwaomba watumishi kuwa na subira wakati serikali ikiendelea zoezi la kuyahakiki ili kuweza kulipa deni sahihi inalodaiwa.

Awali akisoma taarifa ya Idara ya afya kwa Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk. Japhet Simeo amesema idara ya afya inakabiliwa na madeni ya watumishi ambayo ni sh. milioni 109,662,483.

Amesema madeni hayo yametokana na likizo, matibabu, uhamisho wa ndani na nje ya wilaya, gharama za mizigo kwa watumishi waliostaafu, ambapo  halmashauri imejipangia utaratibu wa kulipa madeni hayo pindi inapotokea fedha kutoka serikali kuu.

Hata hivyo kasi ya mtiririko wa fedha ni ndogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya maslahi ya watumishi ambapo Halmashauri inawapongeza na kuwapongeza watumishi wa Idara ya afya kwa kuendelea kuwa wavumilivu na kuwahudumia wananchi.

Dk. Simeo amesema halmashauri inawapongeza Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuongeza mapato nchini, ambapo wana matumaini kuwa watumishi wataboreshewa maslahi na stahiki zao ili kuchochea motisha kiutendaji.

Katika hatua nyingine Dk. Simeo alizungumzia upatikanaji wa dawa, alisema ambao  umeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka jana na kufikia asilimia 80 mwaka huu dawa muhimu katika vituo vyote vya kutolea huduma ambavyo viko 32.
Obama: Tulikosea Sana Kuivamia Libya na Kumuondoa Muammar Gaddafi

Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.

Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.

Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.

Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.

Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.
Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.

Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.

Chanzo: BBC

Friday, 18 March 2016

Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi harambee ya shule ya Sekondari ya Iyunga

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee itakafanyika kesho katika ukumbi wa Ubungo Plaza kwa ajili ya kuchangia fedha zitakazowezesha kukarabati mabweni manne ya shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga yaliyoungua hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Nyerembe Munasa Sabi amesema kuwa wameamua kuomba nguvu kutoka kwa wadau wa elimu na watanzania kwa ujumla kujumuika katika kuchangia shule ya sekondari ya ufundi Iyunga ili waweze kukarabati mabweni yaliyoungua kwa moto.

“ Hadi sasa takribani wanafunzi 421 hawana mahala pa kulala kutokana na kuteketea kwa mabweni na kwa kushirikiana na TAMISEMI tumeamua kusitiza masomo kuanzia tarehe11 March hadi tarehe 01 Aprili ili kupisha ukarabati wa mabweni”

“ Tumeanza ujenzi wa baadhi ya miundombinu iliyoteketea na mabweni ikiwa ni jitihada za wadau mbalimbali waliochangia kutoka Mbeya na nawasihi wanambeya wale waliosoma shule ya Iyunga na shule za Mbeya na watanzania kwa ujumla kujitokeza kesho katika harambee hii” Alisema

Mhe. Nyerembe Munasa Sabi aneongeza kuwa wamepokea michango mbalimbli kutoka kwa wadau wakiwemo Mbeya Cement waliotoa mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na kwa sasa mahitaji yaliyopo ni takribani Shillingi million 770 ili kukarabati na kujenga majengo mapya kwa ajili ya shule hiyo.

Shule ya Sekondari ya  Ufundi Iyunga yenye wanafunzi takribani 9970 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita imekumbwa na majanga ya moto ambayo yamesababisha athari kwa  watoto kutoendelea na masomo na uharibifu wa miundombinu ila Serikali kupitia TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wamejipanga kukusanya  fedha kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa shule hiyo.
Simba aingia jijini  kujeruhi mzee

Simba aliyetoka katika mbuga ya taifa ya wanyama ya Nairobi amemshambulia mzee mmoja jijini humo mapema asubuhi.
Simba huyo alitoka mbugani na kuonekana karibu na eneo la City Cabanas, katika ya Mombasa Road.
Afisa wa mawasiliano wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) Bw Paul Udoto ameambia BBC kwamba mzee aliyejeruhiwa ni wa umri wa miaka 63 na amepewa matibabu ya dharura katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kisha akakimbizwa hospitalini kwa matibabu kamili.
Hata hivyo, Bw Udoto amesema mzee huyo hayuko hatarini.
Kwa mujibu wa afisa huyo, simba huyo huenda alikerwa na kelele za magari yaliyokuwa yakipita.

Vikosi vitatu vya maafisa wa KWS vilitumwa kumdhibiti na kwa mujibu wa Bw Udoto, simba huyo anaelekezwa ndani kwenye mbuga.
Maafisa wanaendelea kushika doria kubaini iwapo kuna simba wengine walitoka mbugani.
Visa vya simba kutoka mbugani vimekuwa vikiripotiwa siku za karibuni. Mwezi mmoja uliopita, simba wanne waliingia maeneo ya makazi eneo la Langata.
Wiki mbili zilizopita, simba wawili walidaiwa kuonekana karibu na barabara ya Ngong.
Raia wa Kenya waishitaki Tanzania

Raia kumi wa Kenya wameituhumu Serikali ya Tanzania, kwa kukamatwa kwa kuwateka jijini Maputo nchini Msumbiji Januari 2006, ambako walikuwa wakiishi kihalali wakitafuta fursa za biashara, na kisha kuwapakiza kwenye ndege ya kijeshi na kuwaleta nchini Tanzania kwa nguvu.
Kwa upande wake, serikali ya Tanzania kupitia mawakili wake imepinga madai hayo na kuitaka mahakama ya Afrika kutupilia mbali maombi ya watuhumiwa. Tanzania inasema watuhumiwa hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuletwa kupitia ndege ya jeshi la Msumbiji.
Wakenya hao wanahoji kuwa kesi yao nchini Tanzania imechukua muda mrefu kwa kuahirishwa mara kwa mara bila sababu. Aidha wanadai kuwa kesi imeendeshwa bila wao kuwa na mawakili wa kuwatetea.
Mawakili wa serikali ya Tanzania pia waliieleza Mahakama ya Afrika kuwa, wawili kati ya raia hao wa Kenya waliofariki wakiwa magereza, walikufa kwa kifo cha kawaida, na kesi iliahirishwa mara kwa mara kutokana na mawakili wa walalamishi kukosa kufika mahakamani siku za kesi.
Wakenya hao walikamatwa miaka kumi iliyopita na kuhukumia kufungwa miaka thelathini jela, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji na ujambazi wa kutumia silaha lililofanyika katika benki ya NMB Tawi la Moshi, mwezi May,2004.
Mahakama ya Africa kuhusu haki za binadamu na za watu iliundwa mwaka 2006 na kuanza kazi zake rasmi mwaka mmoja baadae. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi februari 2016, Mahakama imepokea kesi 74, ambapo 25 kati ya hizo zimekwisha shughulikiwa, huku kesi 4 zikipelekwa katika Tume ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu nchini Gambia.

Monday, 14 March 2016

Merkel ashindwa uchaguzi wa majimbo


Chama cha Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kimeshindwa katika uchaguzi wa majimbo, matokeo ya utafiti wa baada ya uchaguzi yanaonesha.
Matokeo hayo yanaonesha chama cha Christian Democrats kimeshindwa katika majimbo ya Baden-Wuerttemberg naRhineland Palatinate, lakini bado kimeendelea kutawala Saxony-Anhalt.
Chama cha AfD kinachowapinga wahamiaji, kimeimarika pakubwa katika majimbo yote matatu.
Uchaguzi huo ulitazamwa na wengi kama kigezo cha uungwaji mkono wa sera ya Chansela Merkel ya kuwapokea wakimbizi.
Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni moja waliingia Ujerumani mwaka 2015.
Naibu Chansela wa Ujerumani alisema Jumamosi kwamba kuimarika kwa AfD hakutabadili sera za serikali yake kuhusu uhamiaji.
“Huu ni msimamo wazi ambao tutaendelea kuutetea, wa kutetea utu na ubinadamu. Hatutabadili msimamo wetu sasa.”
Lakini mjini Berlin Jumamosi, karibu waandamanaji 2,000 wa mrengo wa kulia walibeba bendera za Ujerumani na kuimba "Merkel sharti aondoke!" na "Sisi ndio watu!"
Pigo hilo kwa Chansela Merkel limetokea siku chache kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Ulaya wa kukamilisha mkataba kati ya EU na Uturuki wa kudhibiti kuingia kwa wahamiaji na wakimbizi.
Mkataba huo, ambao utapelekea wahamiaji wanaowasili nchini Ugiriki wakirejeshwa Uturuki, unakabiliwa na changamoto za kisheria na kisiasa.

Wanasheria wanajizatiti kutafuta mpango ambao utatimiza masharti ya kimataifa kuhusu wakimbizi.
Umoja wa Mataifa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu wametaja mpango huo kuwa usiofuata maadili na haramu.
Ndege ya kivita yatoweka


Umoja wa Milki za Kirabau umesema ndege yake ya moja ya kivita imetoweka ikitekeleza mashambulio dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen.
Shirika la habari la serikali ya nchi hiyo, WAM, lilitangaza kutoweka kwa ndege hiyo bila kutoa maelezo zaidi.
UAE imekuwa ikishiriki katika mashambulio ya muungano wa mataifa yanayoongozwa na Saudi Arabia kutekeleza mashambulio ya angani kumuunga mkono Rais Abedrabbo Mansour Hadi tangu Machi 2015.
Watu 6,000 wameauawa kwenye mapigano nchini Yemen.
Hicho ndicho kisa cha kwanza cha kutoweka kwa ndege ya UAE kwenye mapigano hayo.

Maafisa bado hayajaeleza ndege iliyotoweka ni ya muundo gani na pia iwapo marubani walidhurika.
Jeshi la wanahewa la UAE hutumia ndege za kivita aina ya F-16 na Mirage 2000.
Desemba, ndege aina ya F-16 ya jeshi la Bahrain ilianguka Saudi Arabia kutokana na “hitilafu za kimitambo”, na mwezi Mei ndege ya kivita ya Morocco ilitunguliwa nchini Yemen.
Ndege hizo mbili zilikuwa zikishiriki mashambulio dhidi ya waasi wa Houthi
Erdogan aapa kukabili vikali magaidi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapa kwamba atawakabili vikali magaidi baada ya shambulio la kigaidi kuua watu zaidi ya 36 mjini Ankara.
Bw Erdogan amesema shambulio hilo lililotekelezwa kupitia gari lililotegwa mabomu litazidisha kujitolea kwa maafisa wa usalama wa Uturuki.
Mlipuko huo ulitokea katika kituo muhimu cha uchukuzi cha Guven Park na kujeruhi zaidi ya watu 100. Mshambuliaji mmoja anadaiwa kuuawa.
Waziri wa mambo ya ndani Efkan Ala alisema uchunguzi utakamilishwa Jumatatu na kwamba wote waliohusika watatajwa.
Hakuna kundi lililokiri kuhusika lakini duru za serikali zinashuku chama kilichopigwa marufuku cha Kurdistan Workers Party (PKK).
Utafiti: Tanzania yabainika kuwa nchi ya kwanza isiyo aminifu duniani!



Utafiti umebaini kuwa wananchi wanaoishi kwenye nchi zilizotawaliwa na rushwa nao pia hujikuta wakikosa sifa ya uaminifu.
09M_Honest Table
Utafiti huo umebainisha kuwa uaminifu binafsi huwa mkubwa kwenye jamii zenye matatizo machache ya rushwa, ukwepaji kodi na utapeli wa kisiasa.
Wakati ambapo Austria, Uholanzi na Uingereza zimeshika nafasi ya kwanza katika nchi aminifu duniani, Tanzania na Morocco ambazo ubora wa taasisi zake ulibainika kuwa wa chini, zilifanya vibaya.
Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Nottingham na kuhusisha nchi 159.
Walitumia taarifa zilizopo kuanzia mwaka 2003 za utapeli kisiasa, ukwepaji kodi na rushwa.
Utafiti huo ulibaini kuwa watu wanaoshi kwenye nchi zenye matukio machache ya uvunjaji sheria, walikutwa na uwezekano mdogo wa kudanganya ili kupata fedha ukilinganisha na nchi zenye matatizo ya rushwa.
Ulidai kuwa uwepo wa matukio ya uvunjaji sheria, huwafanya watu kupindisha ukweli.
Chanzo: Daily Mail

Monday, 25 January 2016

China kwenye baridi kali, nyuzi joto ni 4°C, idadi ya waliopoteza maisha je?…Video


Baada ya Marekani kuripotiwa kukumbwa na baridi kali hali iliyopelekea baadhi ya viwanja vya ndege, Barabara na reli kufungwa kwa muda..headlines zimehamia Taiwan.
Wakati Tanzania ikikadiriwa kuwa na nyuzi  38°C na kuendelea kwa sasa, unaambiwa mji wa Taipei uliopo Taiwan umekumbwa na baridi kali huku nyuzi joto ikiwa ni 4°C, joto  ambalo ni dogo na halijawahi kutokea kwa miaka 44 iliyopita.
TAIPEI
Mpaka sasa tayari watu 52 wamepoteza maisha kutokana na kushindwa kuhimili baridi kali…wengi wao wakiwa wameugua nimonia pamoja na maradhi ya moyo.
Watalii zaidi ya 60,000 pia wamekwama Korea Kusini kutokana na baridi kali, pia safari za ndege zimesimama kwa muda.
CH
Miji mingine iliyoathirika ni Hong Kong na Japan.

Thursday, 21 January 2016

Bomu lalipuka katika mgahawa Somalia


Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika ufukwe wa bahari katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu,kulingana na maafisa wa polisi.
Walioshuhudia wamemwelezea mwandishi wa BBC Ibrahim Aden kwamba gari hilo lililojaa vilipuzi liligonga mgahawa huo maarufu wa Lido Beach kabla ya watu watano kujitokeza na kuanza kufyatua risasi.
Haijulikani iwapo kumekuwa na majeruhi.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo,lakini kundi la Alshabaab ndilo linaloshukiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengine kama hayo hapo awali.

Mgahawa wa Lido Beach uliopo pembezoni mwa Mogadishu,huwavutia maelfu ya vijana wa Somalia wanaojifurahisha.
Migahawa kadhaa imefunguliwa katika ufukwe huo katika miaka ya hivi karibuni.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Meja Abdiqadir Ali amekiambia chombo cha habari cha reuters kwamba shambulio hilo lilitokea katika lango la mgahawa huo.
Amesema kuwa uchunguzi unaendelea.