Tuesday, 23 August 2016

Yanga wamekuwa walaini kwa TP Mazembe, waaga michuano

Yanga ilipata pigo dakika mbili baada ya kuruhusu goli, Andrew Vicent ‘Dante’ alioneshwa kadi nyekundu na kuiacha Yanga ikicheza pungufu
Safari ya wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi Yanga leo imefikia mwisho kwa kipigo cha mabao 3-1, dhidi ya TP Mazembe.
Yanga imehitimisha safari hiyo kwa kumaliza nafasi ya misho kwenye Kundi A, huku ikijikusanyia pointi nne na sasa inarudi nyumbani kuendelea na msimu mpya wa Ligi ya Vodacom ambayo tayari imeanza wikiendi iliyopita na yenyewe itashuka dimbani Agosti 28 dhidi ya African Lyon.
Yanga iliyowakosa nyota wake sita wa kikosi cha kwanza iliuanza mchezo huo kwa kufanya mashambulizi mengi lakini ilijikuta ikipachikwa bao la kwanza dakika ya 28, kupitia kwa Bolingi, aliyemalizia pasi nzuri ya Ranford Kalaba.
Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuichanganya Yanga na dakika mbili baadaye ilijikuta ikicheza pungufu baada ya beki wake Andrew Vicent ‘Dante’ kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 30, kwa kumchezea vibaya Kalaba.
Pamoja na kucheza pungufu Yanga walionyesha kupambana na kutengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia huku mshambuliaji wake Amissi Tambwe akikosa msaada kutokana na mbele kubaki peke yake.
Mazembe walirudi kwa kasi kipindi cha pili na katika dakika ya 56, ilipata bao la pili kupitia kwa Kalaba na mshambuliaji huyo aliyeikosa mechi ya Dar es Salaam alifunga bao la pili dakika ya 64 akimalizia pasi nzuri ya Kasusula.
Pamoja na mabao hayo kuingia mfululizo Yanga hawakukata tamaa waliendelea kupambana huku wakifanya mashambulizi ya kustukiza na dakika ya 72 walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi baada ya Amis Tambe kumalizia mpira uliogonga mwamba wa juu ambao ulipigwa na Haruna Niyonzima.
Matokeo hayo yanaipa Mazembe fursa ya kuongoza Kundi A kwa kufikisha pointi 13, na kufuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali huku mshindi wa pili wa kundi hilo akitarajiwa kujulikana baada ya moda mchache katika mchezo ambao Medeama na MO Bejai wanapambana huko Algeria.

Thursday, 14 July 2016

Man Utd nambari tano kwa utajiri duniani

Klabu ya Manchester United imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani na jarida la Forbes, thamani yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba.
Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.
United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn).
Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn).
United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa sana na mkataba wao wa £750m na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika 25 bora.
Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool (41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo.

Tuesday, 3 May 2016

Picha: Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye uwanja wa mazoezi wa Leceister City leo asubuhi
Timu ya Leceister City ambao ni mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uingereza leo asubuhi ilirejea mazoezini baada ya mapumziko ya siku moja.
33C8B6FC00000578-3570857-image-a-82_1462273713634
Wachezaji wa Leicester City wameonekana wakiwa na furaha mazoezini baada ya jana usiku mchezo wa Chelsea dhidi ya Tottenham kuwapa pointi muhimu Leceister City kuwa mabingwa wapya wa Uingereza kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ilipoanzaishwa mwaka 1884.
Leceister City imebakisha mechi mbili, kati ya Chelsea na Everton ili kumaliza ligi kuu msimu huu na hata kama wakifungwa mechi zote mbili zilizobaki timu hiyo haina cha kupoteza.
Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wa Leceistaer City wakiwa mazoezini.
33C5F94800000578-3570857-Leicester_striker_Jamie_Vardy_heads_off_to_training_in_a_white_M-a-31_1462267860274
Mshambuliaji wa Leceister City, Jamie Vardy akiwasili mazoezini
33C735DC00000578-3570857-image-m-46_1462269122513
33C7A35700000578-3570857-image-a-74_1462271826225
33C687B900000578-3570857-image-a-33_1462268163675
Muonekano mpya wa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa King Power
33C7230200000578-3570857-image-m-40_1462268682724
Kocha wa Leceister City, Claudio Ranieri akiwasili mazoezini na kiatu chake kipya kilichoandikwa Champion
33C7A03300000578-3570857-image-a-75_1462271838483
33C8B6FC00000578-3570857-image-a-82_1462273713634
33C716B700000578-3570857-image-a-35_1462268265055
Kepteni wa Leicester City, Wes Morgan akiwasili mazoezini

Thursday, 21 April 2016

Farid Mussa apata zali nchini Hispania

Mchezaji wa Azam FC, Farid Mussa ameitwa Hispania kufanya majaribio.
FARID MUSSA
Farid Mussa ni mmoja kati ya wachezaji chipukizi ambao wanafanya vizuri na timu yake ya Azam FC na timu ya taifa ya Tanznia.
Farid amepata nafasi hiyo ya kwenda Hispania kufanya majaribio kwenye timu za Malaga na Las Palmas ambazo zote zinashiriki ligi kuu ya nchi hiyo (La Liga) na atakuwa huko takribani kwa mwezi mmoja na atarejea Tanzania, May 19.
Mchezaji huyo bado yupo nchini Tunisia na timu yake ya Azam FC lakini Farid kesho Ijumaa ataondoka kuelekea Hispania akitokea huko huko Tunisia.
Kila la kheri Farid Mussa, wewe ni mmoja wa wachezaji ambao tunawategemea kuja kuipandisha timu yetu ya taifa.
Droo ya Kombe la Shirikisho Afrika imefanyika, Yanga kapangwa na klabu yenye miaka 39


Baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya usiku wa April 20 2016 na klabu ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya goli 2-1, sasa wanajiandaa kurudi kucheza Kombe la shirikisho barani Afrika katika hatua ya 16.
Yanga imepangwa kucheza na klabu ya Grupo Desportivo Sagrada Esperança ya Angola katika hatua ya 16 bora ambapo mechi zitachezwa nyumbani na ugenini na baada ya hapo timu nane zitaingia katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Kombe la shirikisho barani Afrika, Grupo Desportivo Sagrada Esperança ilianzishwa December 22 1976 .
gfd
Yanga ataanza kucheza nyumbani kati ya Mei 6-8 na mechi za marudiano zitachezwa kati ya Mei 16-18 2016

Tuesday, 19 April 2016

Cristiano Ronaldo anahamia PSG? kuna haya mapya yameandikwa leo April 19 2016



Headlines za staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kuhusishwa kutaka kuhama Real Madrid na kutaka kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa zimerudi tena katika mitandao.
Awali Ronaldo aliwahi kuhusishwa kutaka kujiunga na PSG ila leo April 19 2016 stori kutoka 101greatgoals.com wameripoti kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi mara tano, stori zinaeleza kuwa Jose Mourinho huenda akajiunga na PSG pamoja na Ronaldo msimu ujao.
Taarifa za Ronaldo kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi zimevuja baada ya Ronaldo kudaiwa kuonekana akiwa Paris Ufaransa kwa ndege ya kukodi na kupelekwa katika hoteli aliyopo Nasser Al-Khelaifi na siku inayofuatia Ronaldo anadaiwa kuondoka na ndege binafsi tena kuwahi mazoezi ya Real Madrid. Huenda kukawa kuna kitu kinaendelea kwani Ronaldo amekuwa akionekana Paris mara kadhaa sasa.

Monday, 14 March 2016

Mbeya City Waifuata Africans Sports Jijini Tanga



Kikosi  cha Mbeya City FC tayari kipo jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya African Sports  unaotajia kuchezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga hii leo.
Mapema jana mkuu wa kitengo cha utabibu kikosi Dr Joshua Kaseko amesibitisha kuwa  wachezaji wote 18 walisafiri kutoka jijini Mbeya tayari wa mchezo huo wako kwenye hali nzuri kabisa na ana imani kubwa watacheza kwenye kiwango bora  ili kuipatia matokeo timu yao hii leo.
“Joseph Mahundi alipata majeraha  kwenye mchezo uliopita, hivi sasa yuko vizuri na tunatarajia  atakuwa sehemu ya kikosi, hakuna shaka kuwa  City iko hapa Tanga  kwa sababu ya kupata matokeo na  hakuna  jambo lingine, tumetoka  kushinda dhidi ya Stand  United  jambo linalotupa nguvu ya kupambana hapo kesho, tuna morali ya hali ya juu kikosini  ambapo kila mmoja  ana  hamu ya kurudi na pointi tatu” alisema.
Kwa upande wake  Kocha Kinnah Phiri ameweka wazi kuwa japo hali ya hewa ya hapa ni tofauti kabisa na ile iliyopo jijini Mbeya lakini hiyo siyo sababu ya City kukosa ushindi mbele ya Africans Sports.
“Hali ya hewa ya hapa ni tofauti sana na iliyopo jijini Mbeya, hilo hatulitizami sana, tumejiandaa vya kutosha, jana asubuhi tulimaliza mazoezi na wachezaji wamepewa muda wa kuweka miili yao sawa kwa kuoga kwenye barafu, hakuna shaka yeyote kuwa  tunazo pointi tatu kutoka hapa” alisema.
Mbeya City wanaelekea katika mchezo wa hii leo huku wakiwa na kumbu kumbu ya kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri, katika mchezo wao uliopita dhidi ya Stand Utd.

Friday, 3 July 2015

Mkataba wa Hamis Kiiza na Simba uko hapa mtu wangu…



Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Uganda Hamisi Kiiza amefanikiwa kufuzu vipimi vya afya yake na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
Kiiza alitua jana nchini akitokea kwao Uganda na leo kusaini mkataba baada ya kufuzu vipimo vya afya yake.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga amesema amekuja kufanya kazi na Simba na kuahidi makubwa akiwa na timu hiyo.

Friday, 5 June 2015

liwahi kusikia chochote kati ya Blatter na Cristiano Ronaldo?? Mwanamke huyu katajwa kuwa ni sababu..

Hali bado sio shwari kwa upande wa Rais wa FIFA, Sepp Blatter… Zimepita siku chache tu tangu atangaze kwamba ataachia ngazi kwenye uongozi wa taasisi hiyo kubwa ya soka duniani kutokana tuhuma za rushwa kuiandama taasisi hiyo.
Leo hii zimetoka taarifa nyingine ambazo zimeibua tetesi za siku nyingi kwamba Rais huyo wa FIFA alikuwa hana uhusiano mzuri na mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo.
Gazeti lenye heshima ndani ya Spain, El Mundo limeripoti kwamba aliyekuwa mchumba wa Ronaldo, Irina Shayk alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Sepp Blatter katika vipindi viwili tofauti.
El Mundo linaripoti kwamba Blatter alikuwa na uhusiano muda mrefu na Mrembo huyo wa kirusi baada ya kuachana na mcheza tennis Ilona Boguska lakini hiyo ilikuwa ni kabla ya kukutana na mwanamama  Linda Barras.
Cristiano Ronaldo na Irina Shayk wakati wa mahusiano yao
Habari hiyo ya Irina na Blatter imeandikwa kwenye na mwandishi wa gazeti la El Mundo, Rosalia Sanchez amesema kwamba taarifa hiyo ya siri ya mahusiano ya Irina na Mzee Blatter ilipata kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika wakati anafanya uchunguzi wa taarifa za rushwa na mahusiano zinamhusu boss huyo wa FIFA.
Uhusiano wao inasemekana ulianza mwaka 2002, wakatengana na kuja kuendelea tena mwaka 2014, wakati Irina akiwa bado na uhusiano na Cristiano Ronaldo ambaye walianza mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa mwaka huu walipotangaza kuachana.
Taarifa ya uhusiano ya Blatter na Irina pia imeripotiwa katika vyombo vya habari vya nchi za Peru, Portugal, Mexico na Vietnam pamoja na kuvuta wmijadala ya watu wengi kwenye mitandao ya kijamii.
Msemaji wa Irina Shayk kaulizwa juu ya tuhuma hizi ila hakujibu chochote..
Bye Bye Filippo “Pippo” Inzaghi


Uongozi wa klabu ya AC Milan umethibitisha taarifa za kumtimua meneja wao wa sasa Filippo “Pippo” Inzaghi na kuanza kumsaka mbadala wake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya nchini Italia (Sirie A).
Inzaghi ataondoka San Siro baada ya kukiongoza kikosi cha AC Milan kwa muda wa mwaka mmoja na imeonekana ameshindwa kutimiza wajibu wa kufikia lengo lililokua linakusudiwa na viongozi wa The Rossoneri baada ya kumaliza katika nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi.
Maamuzi ya kutimuliwa kwa Inzaghi ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo kama mchezaji kuanzia mwaka 2001–2012, yanatarajiwa kufanyika ndani ya juma hili baada ya pande hizo mbili kufanya makubaliano maalum.
Hata hivyo mpaka sasa haijafahamika ni nani atakayeirithi mikoba ya kukindesha kikosi cha AC Milan kwa msimu ujao baada ya aliyekua meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti kukataa kurejea klabuni hapo huku uongozi wakimkana Sinisa Mihajlovic ambaye alikua akiitumikia klabu ya Sampdoria msimu uliopita.
Dino Zoff Aihurumia Juventus Kuelekea Game Ya Barcelona



Gwiji wa soka nchini Italia Dino Zoff, amekiri kuwahurumia mabingwa wa soka nchini humo Juventus, kuelekea katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona utakaochezwa kesho mjini Berlin nchini Ujerumani.
Zoff ambaye aliitumikia Juventus kama mchezaji kuanzia mwaka 1972–1983 kabla ya kuajiriwa kama meneja mwaka 1988–1990 amesema kutokuwepo kwa beki wa kutumainiwa wa klabu hiyo Giorgio Chiellini, ndiyo kunampa wasi wasi na kuwahurumia The Bianconeri.
Chiellini, hatokuwepo katika mchezo huo wa fainali, baada ya kubainika maumivu wa misuli ya paja aliyoyapata wakati akiwa mazoezini juzi jioni hayatoweza kupona katika kipindi cha masaa kadhaa kuelekea katika mchezo dhidi ya FC Barcelona.
Zoff ambaye alikua mlinda mlango mahiri amesema, ni pigo kubwa sana kwa Juventus kwa kumkosa beki huyo ambaye ameonekana kuwa imara wakati wote wa msimu, hivyo ameshauri kutazamwa upya kwa mbinu mbadala za kuweza kuizuia safu ya ushambuliaji wa FC Barcelona.
Hata hivyo gwiji huyo ameonyesha kuwa na matumaini hafifu na beki aliyesalia kwa sasa Andrea Barzagli ambaye anapewa nafasi kubwa wa kuwa mbadala wa Chiellini katika mchezo huo.
Amesema mara kadhaa meneja wa sasa wa Juventus, Massimiliano Allegri, alimtumia Bazagli kama mchezaji wa akiba, hivyo kuanza kwake hiyo kesho na kutarajiwa kucheza kwa muda wa dakika 90 ama zaidi itakua shughuli ya ziada.
Andrea Barzagli, naye alikua katika hatua ya kujiuguza majeraha aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya SSC Napoli majuma mawili yaliyopita na siku mbili zilizopita alithibitishwa kuwa fit kwa ajili ya kuapambana katika mchezo dhidi ya FC Barcelona.
Wakati huo huo Dino Zoff ametabiri kikosi kitakachoanzishwa hiyo kesho katika mchezo wa hatua ya fainali dhidi ya FC Barcelona ambapo anatarajiwa wachezaji hawa watakua changuo la kwanza la meneja Allegri:
Buffon, Ogbonna, Pogba, Pepe, Marchisio, Morata, Tevez, Coman, Llorente, Barzagli, De Ceglie, Bonucci, Padoin, Pirlo, Vidal, Lichtsteiner, Sturaro, Storari, Matri, Evra,Rubinho, Pereyra.

No Comments Yet.

Wednesday, 16 July 2014

DIEGO COSTA AMUAHIDI MOURINHO MATAJI BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MITANO CHELSEA


MSHAMBULIAJI Diego Costa amepania kushinda mataji zaidi baada ya kukamilisha usajili wake Chelsea.
Mzaliwa huyo wa Brazil, aliiwezesha Atletico Madrid kutwaa taji la La Liga msimu uliopita, na kuifikisha Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya walipofungwa na Real Madrid.
Jose Mourinho alishindwa kutwaa taji lolote katika msimu wake wa kwanza wa kurejea Stamford Bridge, lakini Costa anajiamini anaweza kumsaidia kutimiza ndoto hizo baada ya kutua magharibi mwa London.  
d

"Nina furaha sana kusaini Chelsea. Kila mtu anajua ni klabu kubwa katika livi ya ushindani sana, na ninavutiwa sana kuanza Ligi Kuu England na kocha babu kubwa na wachezaji wenzangu. Nikiwa nimecheza dhidi ya Chelsea msimu uliopita ninafahamu ubora wa kikosi ninachojiunga nacho,"amesema mchezaji huyo wa Hispania, anayetua Chelsea kwa dau la Pauni 32 kwa Mkataba wa miaka mitano.
Taarifa ya Chelsea imesema; "Klabu ya Chelsea inayo furaha kutangaza kwamba Diego Costa leo amekamilisha uhamisho wake kutoka Atletico Madrid kwa kusaini Mkataba wa miaka mitano. Atajiunga na kikosi cha kwanza wiki ijayo kwa ajili ya ziara ya Ulaya kujiandaa na msimu," .

Wednesday, 11 June 2014

HUYU HAPA NDO MBADALA WA PWEZA KATABIRI BRAZILI ITASHINDA CHECK VIDEO YA KOBE MTABIRI
Wakati fainali za kombe la dunia zikianza kesho nchini Brazil, mashabiki wa soka nchini Brazil kwa kuipa nafasi kubwa timu yao ya taifa kufanya vyema katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia uliopangwa kuchezwa Arena de São Paulo huko mjini São Paulo. Mmoja wa mashabiki wa soka nchini Brazil ameibuka na harakati za ubashiri kwa kutumia kasa huku akikumbushia katika fainali za mwaka 2010 ambapo ubashiri wa michezo kadhaa ya fainali hizo ulimuhusisha Pweza Paulo. Kasa huyo aliebatizwa jina la The Loggerhead Turtle, *Big Head*, amebashiri mchezo huo wa ufunguzi akiwa katika bwawa la kuogelea ambapo kigezo kikubwa kinachotumika anawekewa samaki kwenye pande mbili zilizo na bendera za nchi zinazoshinda. Ubashiri wa kiumbe huyo unaaminiwa pale anapochagua kula samaki wa upande wenye bedera ya nchi fulani ambapo inaaminika upande huo ndio utakaoibuka na ushind

Monday, 9 June 2014

Fedha zawapandisha ndege Cameroon kwenda Brazil

Mshambuliaji wa Chelsea na nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon ataiongoza timu yake ya taifa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia Brazil.
Mshambuliaji wa Chelsea na nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon ataiongoza timu yake ya taifa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia Brazil.
Hatimaye wachezaji wa Cameroon wako njiani kuelekea kwenye mashindano ya Kombe la Dunia baada ya kukataa kupanda ndege mwanzoni kwenda Brazil kwa sababu ya kutokubaliana na kiasi cha posho.
Ila hatimaye wamekubaliana kiasi hicho cha fedha na shirikisho la mpira wa miguu la nchi hiyo baada ya mkutano wa dharura.
Kocha wa timu Volker Finke alisema wachezaji walikuwa wakilalamikia kwamba dola 61,000 (mil. 102 za kitanzania) ambazo walitakiwa kulipwa kwa ajili ya Kombe la Dunia zilikuwa hazitoshi.
Hakuna mtu anayetosheka na pesa, hata Samuel Eto’o ambaye ni tajiri wa kutupwa?
Timu ya Cameroon ina wachezaji wakubwa na wadogo ambao hata kiuchumi wamepishana kulingana na ligi kila mchezaji anayeichezea, hivyo suala hili lazima lisimamiwe na timu nzima kwa ajili ya maslahi ya taifa kijumla.
Tusiwashangae, mana wasipokomalia hizo pesa zitaishia kwenye midomo ya viongozi walafi tu.
Cameroon wapo kundi A, wakiwa na wenyeji Brazil, Croatia, na Mexico.

Thursday, 5 June 2014

Cristiano Ronaldo ‘arogwa’ na mganga kutoka Ghana

Mganga Kwaku Bonsam kutoka Ghana ameibuka na kudai kuhusika na majeraha yanayomwandama Mreno Cristiano Ronaldo.
Mganga Nana Kwaku Bonsam kutoka Ghana ameibuka na kudai kuhusika na majeraha yanayomwandama nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo.
Nyota huyo wa Real Madrid anasumbuliwa na matatizo ya misuli na kumfanya akose mechi za kirafiki a Kombe la Dunia dhidi ya Mexico na Ireland, Mganga Nana Kwaku Bonsam amedai anahusika na matatizo ya mshindi huyo wa Ballon d’Or, akidai kuwa ni tatizo la kiroho.
“Najua majeraha ya Cristiano Roanaldo yanasababishwa na nini, na nalifanyia kazi hilo”, mganga huyo alikiambia kituo cha redio cha Ghana cha Angel FM.
“Sitanii kuhusiana na hili. Wiki iliyopita, nilitafuta mbwa wanne na kuwatumia kutengeneza roho maalumu inayoitwa “Kahwiri Kapam’.
“Miezi minne iliyopita nilisema kuwa nitashumghulikia Cristiano Ronaldo na kumfanya asicheze Kombe la Dunia au asicheze mechi dhidi ya Ghana na jambo lingine zuri ni kumfanya apone majeraha yake”, aliongeza mganga huyo.
“Kamwe hawezi kutibiwa na daktari, maana hatoweza kupona kwani chanzo cha majeraha yake ni tatizo la kiroho. Leo ni kwenye goti lake, kesho ni paja, kesho kutwa ni tatizo jingine”.
Ghana watacheza na Ureno Juni 26 mjini Brasilia, ambapo itakuwa ni mechi za mwisho ya Kundi G, ambalo linahusisha timu ya Ujerumani na Marekani.
BONANZA LA 9 WANAHABARI KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA JUNI 28 JIJINI ARUSHA


Arusha.Bonanza  la waandishi wa habari na watangazaji Kanda ya Kaskazini linatarajiwa kufanyika june 28 katika viwanja vya General tyre  jijini Arusha na kushirikisha zaidi na wanahabari 150 na wadau wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha  , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma, alisema maandalizi muhimu ya Bonanza yameanza.
Juma alisema bonanza hilo,ambalo huandaliwa na TASWA Arusha na kampuni ya MS UniquePromotion litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari wa michezo mkoa wa Arusha,  ambayo itashirikisha baadhi ya wajumbe wa kamati ya tendaji ya TASWA Taifa.
Hata hivyo alisema bado TASWA Arusha na kampuni ya MS Unique wanatafuta wadhamini wa bonanza hilo ambalo litakuwa ni la tisa kufanyika.
Juma alisema hivi karibuni wadhamini wa bonanza hilo, watatangazwa sambamba na zawadi kwa washindi.

Alisema katika tamasha hilo, wanahabari na wadau wa habari watashiriki katika michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia,mpira wa pete, kukimbiza kuku na kucheza muziki.

Katika tamasha la mwaka jana, hakukuwa na bingwa wa soka baada ya TASWA Dar es Salaam na timu ya chuo cha Uandishi wa habari(AJTC) kushindwa kufungana na kuamua kugawana sehemu ya zawadi iliyokuwa imepangwa.
Kwa upande wa mpira wa pete TASWA Dar es Salaam, alishinda, huku katika mchezo wa kukimbiza kuku TASWA Arusha ilishinda na katika kamba timu ya Sunrise ilishinda wakati timu ya radio 5 na Arusha one zilitamba katika mbio za magunia.
Timu ya Waandishi na watangazaji toka mkoa wa Manyara ya ORS ilishinda zawadi ya timu yenye nidhamu,timu nyingine zilizoshiriki ni Wazee Klabu,Pespi,TBL na timu  ya Kitambi noma.

Wednesday, 4 June 2014

Video: Lampard aanza kuaga Stamford Bridge
Kiungo wa Uingereza Frank James Lampard amesema hana budi kufanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye klabu ya Chelsea na kwenda kusaka maisha mengine nje ya nchi yake. Frank Lampard amesema imemuuwia vigumu kufanya maamuzi ya kuachana na klabu ya Chelsea ambayo ameitumikia kwa miaka 13 tena kwa mafanikio makubwa. Amesema anajua kuondoka kwake hakutoathiri jambo lolote ndani ya klabu hiyo ya jijini London, hivyo amewataka mashabiki wake kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho amesisitiza hana budi kuondoka. Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35, amesema suala la kuondoka kwenye klabu ya Chelsea katu haliwezi kumuathiri katika maandalizi ya kujiandaa na fainali za kombe la dunia ambapo kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kimeweka kambi mjini Miami nchini Marekani. Wakati huo huo Frank James Lampard anatarajia kuiongoza timu yataifa ya Uingereza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ecuador ambao utachezwa hii leo huko nchini Marekani. Lampard amesema amefurahishwa na hatua ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson kumpa heshima ya kuwa nahodha katika mchezo huo, ambao utakuwa mchezo wa pili wa kujiandaa na fainali za kombe la dunia baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Peru mabao matatu kwa sifuri mwishoni mwa juma lililopita. Katika hatua nyingine kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amesema kambi ya kikosi chake inaendelea vizuri na ana hakika mchezo wa hii leo utakisaidia kikosi chake kikamilifu katika harakati za kuelekea nchini nchini Brazil. Amesema hali ya wachezaji wote mpaka sasa ni shwari na ana hakika wote watakwenda nchini Brazil wakiwa na afya njema tayari kwa mapambano ya kurejea historia ya mwaka 1966 ambapo ilikuwa mwanzo na mwisho kwa Uingereza kutwaa ubingwa wa dunia.
Tizama:WALICHOFANYIWA PANONE FC MARA BAADA YA KUPANDA LIGI DARAJA LA KWANZA .


Msafara wa magari ukiongozwa na mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro Goodluck Mushi wakipita katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi mara baada ya kuwasili wakitokea jijini Mbeya ambako timu hiyo imefanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza.
Wachezaji wakishuka katika basi la Hood baada ya kuwasili mjini Moshi.
Furaha ilikuwa kubwa katika eneo hilo mara baada ya timu kuwasili.
Kama vile viongozi wa timu hawaamini kuwa wako katika ardhi ya nyumbani Moshi .
Wachezaji wengine walikuja kupokelewa na wazazi wao.
Baadhi ya wachezaji wakiwa nje ya jengo la Posta katikati ya mji wa Moshi walipoteremka mara baada ya kurejea wakitokea mkoani Mbeya.
Katibu  wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)Mohamed Musa(mwenye suti) akiteta na viongozi wengine waliofika katika mapokezi ya timu hiyo akiwemo mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Hai,Harold Kifunda(mwenye begi)
Meneja wa kampuni ya Panone Ltd kanda ya kaskazini Gido Marandu akiwa na mwandishi wa habari za Michezo wa kituo cha radio cha Moshi fm wakibadilishana mawazo katika hafla ya chakula cha mchana katika mgahawa wa Fresh Coach muda mfupi baada ya mapokezi.
Makocha wa timu ya Panone fc ,Jumanne Ntambi na Atuga Manyundo wakiteta jambo wakati wa chakula cha mchana kwa timu hiyo katika Mgahawa wa Fresh Coach.
Wachezaji wa klabu ya Panone fc ya mkoani Kilimanjaro wakiwa katikaMgahawa wa Fresh Coach wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na uongozi wa Kampuni ya Panone Ltd.