Gwiji wa soka nchini Italia Dino Zoff, amekiri kuwahurumia mabingwa
wa soka nchini humo Juventus, kuelekea katika mchezo wa hatua ya
fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona
utakaochezwa kesho mjini Berlin nchini Ujerumani.
Zoff ambaye aliitumikia Juventus kama mchezaji kuanzia mwaka 1972–1983 kabla ya kuajiriwa kama meneja mwaka 1988–1990 amesema kutokuwepo kwa beki wa kutumainiwa wa klabu hiyo Giorgio Chiellini, ndiyo kunampa wasi wasi na kuwahurumia The Bianconeri.
Chiellini, hatokuwepo katika mchezo huo wa fainali, baada ya kubainika maumivu wa misuli ya paja aliyoyapata wakati akiwa mazoezini juzi jioni hayatoweza kupona katika kipindi cha masaa kadhaa kuelekea katika mchezo dhidi ya FC Barcelona.
Zoff ambaye alikua mlinda mlango mahiri amesema, ni pigo kubwa sana kwa Juventus kwa kumkosa beki huyo ambaye ameonekana kuwa imara wakati wote wa msimu, hivyo ameshauri kutazamwa upya kwa mbinu mbadala za kuweza kuizuia safu ya ushambuliaji wa FC Barcelona.
Hata hivyo gwiji huyo ameonyesha kuwa na matumaini hafifu na beki aliyesalia kwa sasa Andrea Barzagli ambaye anapewa nafasi kubwa wa kuwa mbadala wa Chiellini katika mchezo huo.
Amesema mara kadhaa meneja wa sasa wa Juventus, Massimiliano Allegri, alimtumia Bazagli kama mchezaji wa akiba, hivyo kuanza kwake hiyo kesho na kutarajiwa kucheza kwa muda wa dakika 90 ama zaidi itakua shughuli ya ziada.
Andrea Barzagli, naye alikua katika hatua ya kujiuguza majeraha aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya SSC Napoli majuma mawili yaliyopita na siku mbili zilizopita alithibitishwa kuwa fit kwa ajili ya kuapambana katika mchezo dhidi ya FC Barcelona.
Wakati huo huo Dino Zoff ametabiri kikosi kitakachoanzishwa hiyo kesho katika mchezo wa hatua ya fainali dhidi ya FC Barcelona ambapo anatarajiwa wachezaji hawa watakua changuo la kwanza la meneja Allegri:
Buffon, Ogbonna, Pogba, Pepe, Marchisio, Morata, Tevez, Coman, Llorente, Barzagli, De Ceglie, Bonucci, Padoin, Pirlo, Vidal, Lichtsteiner, Sturaro, Storari, Matri, Evra,Rubinho, Pereyra.

0 comments: