Tuesday, 23 August 2016

Yanga wamekuwa walaini kwa TP Mazembe, waaga michuano

Yanga ilipata pigo dakika mbili baada ya kuruhusu goli, Andrew Vicent ‘Dante’ alioneshwa kadi nyekundu na kuiacha Yanga ikicheza pungufu
Safari ya wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi Yanga leo imefikia mwisho kwa kipigo cha mabao 3-1, dhidi ya TP Mazembe.
Yanga imehitimisha safari hiyo kwa kumaliza nafasi ya misho kwenye Kundi A, huku ikijikusanyia pointi nne na sasa inarudi nyumbani kuendelea na msimu mpya wa Ligi ya Vodacom ambayo tayari imeanza wikiendi iliyopita na yenyewe itashuka dimbani Agosti 28 dhidi ya African Lyon.
Yanga iliyowakosa nyota wake sita wa kikosi cha kwanza iliuanza mchezo huo kwa kufanya mashambulizi mengi lakini ilijikuta ikipachikwa bao la kwanza dakika ya 28, kupitia kwa Bolingi, aliyemalizia pasi nzuri ya Ranford Kalaba.
Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuichanganya Yanga na dakika mbili baadaye ilijikuta ikicheza pungufu baada ya beki wake Andrew Vicent ‘Dante’ kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 30, kwa kumchezea vibaya Kalaba.
Pamoja na kucheza pungufu Yanga walionyesha kupambana na kutengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia huku mshambuliaji wake Amissi Tambwe akikosa msaada kutokana na mbele kubaki peke yake.
Mazembe walirudi kwa kasi kipindi cha pili na katika dakika ya 56, ilipata bao la pili kupitia kwa Kalaba na mshambuliaji huyo aliyeikosa mechi ya Dar es Salaam alifunga bao la pili dakika ya 64 akimalizia pasi nzuri ya Kasusula.
Pamoja na mabao hayo kuingia mfululizo Yanga hawakukata tamaa waliendelea kupambana huku wakifanya mashambulizi ya kustukiza na dakika ya 72 walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi baada ya Amis Tambe kumalizia mpira uliogonga mwamba wa juu ambao ulipigwa na Haruna Niyonzima.
Matokeo hayo yanaipa Mazembe fursa ya kuongoza Kundi A kwa kufikisha pointi 13, na kufuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali huku mshindi wa pili wa kundi hilo akitarajiwa kujulikana baada ya moda mchache katika mchezo ambao Medeama na MO Bejai wanapambana huko Algeria.

Thursday, 14 July 2016

Man Utd nambari tano kwa utajiri duniani

Klabu ya Manchester United imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani na jarida la Forbes, thamani yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba.
Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.
United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn).
Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn).
United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa sana na mkataba wao wa £750m na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika 25 bora.
Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool (41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo.

Tuesday, 3 May 2016

Picha: Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye uwanja wa mazoezi wa Leceister City leo asubuhi
Timu ya Leceister City ambao ni mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uingereza leo asubuhi ilirejea mazoezini baada ya mapumziko ya siku moja.
33C8B6FC00000578-3570857-image-a-82_1462273713634
Wachezaji wa Leicester City wameonekana wakiwa na furaha mazoezini baada ya jana usiku mchezo wa Chelsea dhidi ya Tottenham kuwapa pointi muhimu Leceister City kuwa mabingwa wapya wa Uingereza kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ilipoanzaishwa mwaka 1884.
Leceister City imebakisha mechi mbili, kati ya Chelsea na Everton ili kumaliza ligi kuu msimu huu na hata kama wakifungwa mechi zote mbili zilizobaki timu hiyo haina cha kupoteza.
Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wa Leceistaer City wakiwa mazoezini.
33C5F94800000578-3570857-Leicester_striker_Jamie_Vardy_heads_off_to_training_in_a_white_M-a-31_1462267860274
Mshambuliaji wa Leceister City, Jamie Vardy akiwasili mazoezini
33C735DC00000578-3570857-image-m-46_1462269122513
33C7A35700000578-3570857-image-a-74_1462271826225
33C687B900000578-3570857-image-a-33_1462268163675
Muonekano mpya wa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa King Power
33C7230200000578-3570857-image-m-40_1462268682724
Kocha wa Leceister City, Claudio Ranieri akiwasili mazoezini na kiatu chake kipya kilichoandikwa Champion
33C7A03300000578-3570857-image-a-75_1462271838483
33C8B6FC00000578-3570857-image-a-82_1462273713634
33C716B700000578-3570857-image-a-35_1462268265055
Kepteni wa Leicester City, Wes Morgan akiwasili mazoezini

Thursday, 21 April 2016

Farid Mussa apata zali nchini Hispania

Mchezaji wa Azam FC, Farid Mussa ameitwa Hispania kufanya majaribio.
FARID MUSSA
Farid Mussa ni mmoja kati ya wachezaji chipukizi ambao wanafanya vizuri na timu yake ya Azam FC na timu ya taifa ya Tanznia.
Farid amepata nafasi hiyo ya kwenda Hispania kufanya majaribio kwenye timu za Malaga na Las Palmas ambazo zote zinashiriki ligi kuu ya nchi hiyo (La Liga) na atakuwa huko takribani kwa mwezi mmoja na atarejea Tanzania, May 19.
Mchezaji huyo bado yupo nchini Tunisia na timu yake ya Azam FC lakini Farid kesho Ijumaa ataondoka kuelekea Hispania akitokea huko huko Tunisia.
Kila la kheri Farid Mussa, wewe ni mmoja wa wachezaji ambao tunawategemea kuja kuipandisha timu yetu ya taifa.
Droo ya Kombe la Shirikisho Afrika imefanyika, Yanga kapangwa na klabu yenye miaka 39


Baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya usiku wa April 20 2016 na klabu ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya goli 2-1, sasa wanajiandaa kurudi kucheza Kombe la shirikisho barani Afrika katika hatua ya 16.
Yanga imepangwa kucheza na klabu ya Grupo Desportivo Sagrada Esperança ya Angola katika hatua ya 16 bora ambapo mechi zitachezwa nyumbani na ugenini na baada ya hapo timu nane zitaingia katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Kombe la shirikisho barani Afrika, Grupo Desportivo Sagrada Esperança ilianzishwa December 22 1976 .
gfd
Yanga ataanza kucheza nyumbani kati ya Mei 6-8 na mechi za marudiano zitachezwa kati ya Mei 16-18 2016

Tuesday, 19 April 2016

Cristiano Ronaldo anahamia PSG? kuna haya mapya yameandikwa leo April 19 2016



Headlines za staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kuhusishwa kutaka kuhama Real Madrid na kutaka kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa zimerudi tena katika mitandao.
Awali Ronaldo aliwahi kuhusishwa kutaka kujiunga na PSG ila leo April 19 2016 stori kutoka 101greatgoals.com wameripoti kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi mara tano, stori zinaeleza kuwa Jose Mourinho huenda akajiunga na PSG pamoja na Ronaldo msimu ujao.
Taarifa za Ronaldo kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi zimevuja baada ya Ronaldo kudaiwa kuonekana akiwa Paris Ufaransa kwa ndege ya kukodi na kupelekwa katika hoteli aliyopo Nasser Al-Khelaifi na siku inayofuatia Ronaldo anadaiwa kuondoka na ndege binafsi tena kuwahi mazoezi ya Real Madrid. Huenda kukawa kuna kitu kinaendelea kwani Ronaldo amekuwa akionekana Paris mara kadhaa sasa.