Friday, 22 April 2016

Raymond asimulia alivyopata tabu, ndugu zake walimkatia tamaa baada ya kuona hatoki (Video)

Kabla ya kuchukuliwa WCB, Raymond alikuwa msanii mwenye kipaji ndani ya Tip Top Connection lakini maisha yalikuwa yakimwendea kombo.
12530931_1134578353259492_799030960_n
Ilimlazimu kuvumilia na kusubiria zamu yake ya kutoka kwa muda mrefu kiasi ambacho hata ndugu zake kwao Mbeya walimkatia tamaa na kumsihi arudi tu.
“Namshukuru Mungu kwasababu nilishapata tabu sana. Kuna muda nilikuwa nakaa mwenyewe, sitaki kulia lakini machozi yananitoka kwasababu unapita kwenye situation ngumu, kuna muda unajiona una bahati mbaya,” anasema.
“Kuna watu unawaona kabisa huyu jamaa ananidharau kwasababu alishaniona tangu nahangaika, toka nateseka, kuna dharau zingine ukiziona zinauma. Ni vitu vingi ambavyo nilikuwa nakutana navyo nikivikumbuka.. kuna maneno ambayo nilikuwa nakutana nayo nikiyakumbuka yalikuwa yananiumiza moyo.”
“Ilikuwa wakati mgumu sana kwasababu kuna watu wengine nyumbani ‘wewe ulishaondoka nyumbani hatuoni nyimbo.’ Kwahiyo hadi nyumbani unapigiwa simu, mama, nani, kaka zangu. Nikawa naanza kujiona kama mla unga, yaani watu wamenikatia tamaa.”
Ray anasema ilifika hatua alikataa tamaa na kutaka kurudi Mbeya kiasi cha kumtumia Babutale ujumbe mrefu wa kulalamika uliosababisha wakosane kwa muda.
Anasema kwa sasa maisha yamebadilika kwa kiasi kikubwa kutoka kudharaulika hadi kuanza kuheshimika. Anasema hata mama yake anafurahia hatua aliyopiga.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: