Thursday, 25 August 2016

Wednesday, 24 August 2016

Tuesday, 23 August 2016

Mpiga tarumbeta wa Bob Marley, afariki

Mpiga tarumbeta Headley Bennett, ambaye alishiriki katika wimbo wa kwanza wa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za rege Bob Marley 'Judge Not,' amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Mwanawe Carol Bennett, alithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo siku ya Jumapili.
Carol hakusema sababu maalum ya kifo cha mwanamuziki huyo, lakini alisema babake alikuwa akiugua shinikizo la damu na hivi majusi alipatika na saratani ya kiume.
Bennett alishiriki kwa muziki wa Gregory Isaacs na Jimmy Cliff
Benneth alishiriki na wanamuziki wa nyimbo za rege kama vile Bunny Wailer na Gregory Isaacs.
Alituzwa na serikali ya Jamaica mwaka wa 2005 kama Mjamaica wa sita mwenye hadhi ya juu.
Alichokiandika Raymond wa WCB baada ya kupewa zawadi ya gari


Moja ya headline kwenye mitandao ya kijamii iliyochukua nafasi usiku wa August 22 2016 ni pamoja na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa staa wa bongo flava kutokea katika label ya WCB Raymond ambapo uongozi wake uliamua kumfanyia suprise ya zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4 yenye thamani ya milioni 20 za kitanzania.
Leo August 23 Raymond kupitia ukurasa wake wa instagram aliamua kuyatoa yake ya moyoni kwa kuandika…>>>’Kweli Nimeamini Mungu Hana upendeleo.nilikua mtu nilie jikatia tamaa ndani ya miaka takribani mi nne nilikua nikiangaika na muziki wangu nakushukuru sana sana
‘Kaka Lao Diamond Platnumz Umenifundisha vitu vingi saaaaaanaaa hadi leo naiona njia boss wangu Babu Tale ni mwaka wa tano sasa toka Umenijua umenivumilia kwa mengi hadi leo hii haujanichoka na unanisaidia kwa moyo mmoja’
Boss Sallam Sk Asante sana kwakupigania kila siku thamani ya muziki wangu nakuakikisha nafika sehemu nzuri Mkubwa Fella wewe ni zaidi ya mzazi maana umenilea nakunifundisha meeengi kwenye muziki
‘Madee Sitoacha kukushukuru kaka lao wewe nikioo naamini unafurahi kuniona mdogo wako hapa nilipo maana unanijua saaaaanaaaa

Monday, 25 July 2016