Timu ya Leceister City ambao ni mabingwa wapya wa ligi kuu
ya Uingereza leo asubuhi ilirejea mazoezini baada ya mapumziko ya siku
moja.
Wachezaji wa Leicester City wameonekana wakiwa na furaha mazoezini
baada ya jana usiku mchezo wa Chelsea dhidi ya Tottenham kuwapa pointi
muhimu Leceister City kuwa mabingwa wapya wa Uingereza kwa mara ya
kwanza tangu timu hiyo ilipoanzaishwa mwaka 1884.
Leceister City imebakisha mechi mbili, kati ya Chelsea na Everton ili
kumaliza ligi kuu msimu huu na hata kama wakifungwa mechi zote mbili
zilizobaki timu hiyo haina cha kupoteza.
Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wa Leceistaer City wakiwa mazoezini.
Mshambuliaji wa Leceister City, Jamie Vardy akiwasili mazoezini
Muonekano mpya wa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa King Power
Kocha wa Leceister City, Claudio Ranieri akiwasili mazoezini na kiatu chake kipya kilichoandikwa Champion
Kepteni wa Leicester City, Wes Morgan akiwasili mazoezini
0 comments: