Pata picha unaingia zako supermarket,
unanunua mahitaji mbalimbali ya nyumbani na unajua ukifika home kazi
yako ni moja tu ya kupika, lakini unakutana na vitu vya ajabu.
Muhammad Hussain na mkewe Sanam wanaoishi katika mji wa Birmingham
baada ya kutoka zao Supermarket wakaingia jikoni kwa ajili ya kuandaa
chakula lakini walipofungua nyanya zilizosindikwa kwenye kopo ili
kuzitumia walikuta ndani ina mjusi aliyekufa.
Pamoja na kupeleka malalamiko yao kwa uongozi wa Supermarket hiyo inayoitwa Masala Bazaar inayomilikiwa na Euro Food waliombwa radhi kwa kilichotokea na kuahidiwa kufanyika uchunguzi wa kina kutoka kwa waandaaji kutoka Italy.
Wamesema walinunua makopo 12 ya nyanya na tayari walishatumia saba kati yake hali inayowapa wasiwasi mkubwa wa afya zao.
0 comments: