Headlines nyingine kubwa East Africa ni ishu ya Rais Obama
kutua Kenya July 2015.. alivyokuja TZ bila kwenda kwao Kenya ni kama
watu wa 254 hawakuichukulia poa hivi.. aliahidi atakwenda na kweli
mpango wake unaelekea kukamilika.
Stori nyingine kubwa Kenya ni ishu ya maandalizi ya mapokezi yake, watafanya kama ilivyokuwa TZ au wao itakuwa tofauti??
Headlines kubwa Magazeti ya Nairobi inahusu kutua kwa ndege kubwa ya Kijeshi katika Uwanja wa Jomo Kenyatta, ikiwa na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha unakuwepo wakati ambao Obama atakuwa ndani ya 254.. kati ya vifaa hivyo vingine ni vya Mawasiliano.
Mgeni huyu alipokuja TZ tuliona vingi
sana, barabara zikasafishwa Dar ikawa safi kabisa.. Nitaendelea kukupa
headlines za ujio wa Obama Kenya kila mara mtu wangu baada ya ripota Julius Kipkoech wa millardayo.com kunisogezea updates zote !
0 comments: