Monday, 2 June 2014

Mtoto wa Pele afungwa jela miaka 33 Brazil

Gwiji wa soka Pele akionekana mwenye huzuni.
Gwiji wa soka Pele akionekana mwenye huzuni.
Akiwa na umri wa miaka 43, mchezaji mpira mstaafu, atatumikia kifungo kwa kosa la kujipatia pesa kwa kusafirisha dawa za kulevya, iliripoti BBC.Edinho alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005, ametumikia kifungo kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya, pamoja na kuwa na ushirikiano na wauzaji madawa ya kulevya maarufu katika jiji la Santos.
Kijana huyo wa gwiji Pele alikuwa akiichezea klabu ya zamani ya baba yake ya Santos katika miaka ya 1990.
Edinho, ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mwalimu wa walinda milango (makipa) Santos, iliripotiwa akisema kuwa yeye ni mwathirika wa dawa za kulevya na kukataa mashtaka ya kuwa anasafirisha.
Vyombo vya habari vya Brazil havikuweza kumpata Edinho, ambaye jina lake halisi ni Edson Cholbi do Nascimento. Anatarajiwa kukata rufaa.
Mchawi soka (kama watu wanavyopenda kumuita) Pele akiwa na familia yake.
Mchawi soka (kama watu wanavyopenda kumuita) Pele akiwa na familia yake.
Edinho ni mtoto wa tatu wa kiume wa ndoa ya kwanza ya Pele, na alikuwa na miaka mitano wakati familia ilipohamia New York pamoja na baba yake aliyekuwa akiichezea Cosmos.
Alikuwa mlinda mlango wa Santos mwaka 1995 wakati timu hiyo ilipofikia fainali ya ligi ya Brazil na kupoteza taji kwa Botafogo.
Mwaka 2006, Pele alimtembelea kijana wake gerezani na kusema; “Mungu akipenda, haki itapatikana. Hakuna ushahidi wowote dhidi ya mwanangu.
Pele alishinda Kombe la Dunia la mwaka 1958, 1962 na 1970 na alitajwa kama mchezaji nguli kwenye kizazi chake.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: