Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amesema uchunguzi wa tuhuma
zilizomfanya Rais John Magufuli kumsimamisha kazi jana utabainisha
ukweli huku akihoji; “ikiwa itabainika kwamba nilionewa nitalipwa
fidia?”
Alisema
hayo mara baada ya Dk Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi wakati wa
uzinduzi wa Daraja la NSSF Kigamboni ambalo sasa litaitwa Daraja la
Nyerere baada ya kumwita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
kueleza tuhuma dhidi ya mkurugenzi.
Alipoulizwa
jana, Kabwe alisema hakuwa na taarifa za kusimamishwa kwake na
mazungumzo yake na mwandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Habari mkurugenzi?
Kabwe: Salama.
Mwandishi: Tumepata
taarifa za kusimamishwa kwako kazi na Rais kutokana na tuhuma
zilizotolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda tunaomba
maoni yako. Kabwe: Sijasikia ndiyo kwanza unaniambia wewe, kasema lini Rais?
Mwandishi:Leo wakati akizindua Daraja la Kigamboni. Kabwe: Alitamka palepale au?
Mwandishi: Ndiyo.
Kabwe: Sasa kama ameshasema yeye ndiyo mkubwa mimi sina la kusema tena.
Mwandishi: Nataka kujua unazungumziaje uamuzi huo? Kabwe:
Nimekwambia sina la kukwambia kwa sasa lakini nimesema tu sina shida na
hilo, uchunguzi ufanyike nina uhakika ukweli utajulikana tu. Lakini
kama ukijulikana na ikibainika nimeonewa je, kuna fidia yoyote
nitalipwa?
0 comments: