MTANGAZAJI aliyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse, amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa za kuongeza makalio.Habari za moto kutoka kwa chanzo cha kuaminika, zinasema kuwa Maimartha ambaye pia huitwa Mai amefikia hatua hiyo baada ya yeye kutumia na kufanikiwa.
“Hamshangai siku hizi kila staa anaonekana kuwa na makalio makubwa?
Ni kazi ya Mai hiyo. Anafanya hiyo biashara muda mrefu sana. Ni za
kunywa na kupaka.
“Mbona hata yeye ametumia dawa hizo muda mrefu sana? Ukimwangalia
utagundua zamani hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni kwa sababu ya dawa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Hata Lulu Semagongo (Aunt Lulu) ndiye aliyemsababishia
kuwa na makalio makubwa kwani wakati wako karibu alikuwa akimpa dawa
hizo.”
Waandishi wetu walifika dukani kwa Mai bila kujua kama ni waandishi
na kuulizia bidhaa hizo ambapo zilitolewa, wakapiga picha bila
kugundulika.
Mai
akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa waandishi waliokuwa na njaa ya
habari, aliwaambia: “Ni dawa nzuri, mara moja zinarekebisha umbo na
unakuwa wa kuvutia. Kuna za shilingi 250,000 na 260,000 inategemea kama
ni vidonge au losheni.”
Waandishi wetu walipompigia simu Mai baada ya kutoka dukani hapo na
kumweleza kuhusu uuzaji wa dawa hizo dukani kwake, alisema duka lake
linauza urembo wa aina zote kwa mastaa na wasio mastaa.
“Kama nimetumia dawa za kuongeza makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi
duka langu linadili na urembo wa aina zote,” alisema Mai akishindwa
kufafanua zaidi.
Lulu alipovutiwa waya na kuulizwa kama makalio yake ni matokeo mazuri
ya dawa za Mai alisema: “Sijawahi kutumia dawa za Mai kwa ajili ya
kuongeza makalio. Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa nawaelekeza kwa Mai.”
0 comments: