Unaweza kudhani kuwa mambo haya yapo hapa tzee tu, kumbe ni kila
sehemu, hata huko kwa States yapo, ile show aliyekuwa aifanye mkali wa
Afro Pop kutoka Bongo Diamond platnumz, imeingia dosari, baada ya
promota kushindwa kufikia ahadi zake katika swala zima la mkwanja, Show
hii iliyokuwa ifanyike siku ya ijumaa ya kesho tarehe 30 May mjini
Northampton, ndiyo ishakufa tena baada ya Dangote kuzinguliwa kibongo
bongo.
Diamond Platnumz alifunguka kupitia mtandao wa Instagram na kusema haya
Kutokana na Promoter kushindwa kutimiza makubaliano hadi sasa, imetubidi kukatisha show ya Northampton…! NEW YORK, NEW JERSEY niko njiani tukutane tare 31 ya Mwezi huu!
0 comments: