Saturday, 19 April 2014

SIRI IMEFICHUKA..!! KUMBE ZILE MILIONI 13 ALIZOTOA WEMA KWA AJILI YA KAJALA HAZIKUWA ZA WEMA, HUYU NDIYO MUHUSIKA WA KUTOA PESA HIZO


Siri zimezidi kuvuja juu ya uhasama baina ya mastaa
wawili wa kike bongo. Miss tanzania 2006. Wema sepetu
na kajala masanja. Ambapo inaelezwa kuwa kiasi cha pesa
sh.mil 13. Ambazo wema alimlipia kajala kumuokoa na
hukumu ya kwenda jela katika mahakama ya hakimu mkazi
kisutu dar hazikuwa zake.
kwa mujibu wa watu wa karibu na mastar hao Wema
hakuwa na jeuri ya kutoa fedha hizo ndio maana familia ya
mrembo huyo ilionyesha mshtuko mkubwa kwa binti yao
kutoa pesa za bure kwa mtu baki kama kajala.
Habari zaidi zimesema kwamba kabla wema hajatoa pesa
hizo alimpigia simu mfadhili huyo na kumueleza
kilichokuwa kinaendelea mahakamani hapo ambapo
aliruhusu pesa kutolewa.
kama pesa hiyo ingetoka mfukoni mwa wema basi familia
yake akiwemo mamake asingeweza kumwacha bila
kumuhoji bint yake.lakini mama wema alieleweshwa hali
ilivyo na ndio maana akatulia.pesa ilitolewa na kigogo
huyo ambaye sasa anatoka na kajala.
Aidha mtoa habari huyo alidai kwamba kabla ya wema
kumsaidia Kajala mil.13 hakuwahi kutoa msaada wowote
wa kifedha zaidi ya kula ubwabwa na watoto yatima.
Sani iliwahi kumpa taarifa wema kwamba kulikuwa na
mama anayehitaji msaada wa laki moja kutokana na
matatizo aliyokuwa nayo alijibu kwamba yeye sio serikali
na kumsaidia Kajala kusiwafanye watu wamuone kama
taasisi ya kutoa misaada.
Taarifa zaidi zimedai kwamba kutokana na tabia za
mastaa zilivyo isingekuwa rahisi kwa Wema kutoa hata
senti tano yake!
Naamini kwa hali ya mastaa ilivyo Wema kama wema
asingeweza kutoa hata sh. Mia ili kumtoa kajala.Nyuma ya
kesi ya kajala kulikuwa na huyo kigogo ambaye hivi sasa
pesa zake zote anammwagia kajala.mambo yamegeuka
ndivyo sivyo!” alisema.
Vyanzo vyetu hivyo vilitoa mfano wa msanii mwingine jack
wolper ambaye alimpa msaada wa mil.10 aliyekuwa nyota
wa filam Juma kilowoko au Sajuki kwa ajili ya matibabu na
kudai hazikuwa zake , Wolper hakuwa na uwezo huo pesa
zilikuwa za Dallas ambaye alimtumia Wolper kama kama
bahsha kuufikisha mchango wake. Kiliongea chanzo hicho.
Mwandishi ni Christopher Lissa.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: