Monday, 21 April 2014

RIYAMA NJIA PANDA KWA MITUNGI



Stori: Erick Evarist

Mh! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Riyama Ally, amejikuta akiwa njia panda baada ya kutakiwa kunywa pombe ya kienyeji aina ya ugimbi ambayo hajawahi kunywa maishani mwake.

Riyama aliingia kwenye mtihani huo juzikati pande za Songea alipokuwa amekwenda kikazi ambapo alitakiwa kunywa pombe hiyo kutokana na matakwa ya filamu lakini akashindwa.

“Ulikuwa mtihani kwa kweli, ili kuleta uhalisia ilitakiwa ninywe pombe hiyo lakini kiukweli nilishindwa kwa kuwa sijawahi kunywa hata siku moja, ilibidi nizuge na kopo tupu,” alisema Riyama ambaye ni mkali wa kuzitendea haki sini za siriasi.
GPL
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: