BOOOM! Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili Bongo, mwigizaji Wema Isaac Sepetu na mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wanadaiwa kuipasua familia ya kinara wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu na familia hiyo kuna mgawanyiko ambao umesababisha mpasuko unaofanya familia hiyo kuwa na makundi mawili yasiyoelewana juu ya uhusiano wa Diamond na warembo hao.
Kwa sasa Diamond anatoka kimapenzi na Wema baada ya kumwagana na Penny lakini mtangazaji huyo anadaiwa kuendelea kwenda katika familia hiyo kwani asilimia kubwa inaonesha anakubalika zaidi ya wengine wote.
TEAM PENNY VS TEAM WEMA
Habari zilidai kuwa mpasuko huo ni mkubwa kwani kundi moja linalojiita Team Penny linamkubali zaidi Penny na lingine ambalo lina watu wachache Team Wema linamkubali Wema. Imefahamika kwamba kundi linalomkubali Penny na kumuona ndiye mwanamke sahihi kuwa na Diamond japokuwa wameshaachana ni Mama Diamond mwenyewe, Sanura Kassim ‘Sandra’, dada zake Esma Platnumz, Queen Darleen, Anko na dada wa hiyari wa Diamond, Halima Haroun ‘Kimwana’
Ilidaiwa kwamba kundi hilo limekuwa likitoa ushirikiano wa karibu mno kwa Penny na sehemu nyingi wanakuwa wote ikiwemo kwenye sherehe na viwanja vya starehe, yaani ni fulu kujiachia.
Habari hizo zilidadavua kuwa hata dada wa Diamond, Esma anaishi nyumba moja na wifi yake huyo wa zamani.
“Familia ya Diamond imegawanyika katika makundi mawili, kundi kubwa linamkubali sana Penny japokuwa alishaachana na Diamond. Ilisemekana kuwa si familia tu kwani hata madansa wa Diamond wanampenda sana Penny kuliko Wema,” kilisema chanzo.
TEAM WEMA HII HAPA
Uchunguzi wa wanahabari wetu ulibaini kuwa ndani ya kundi linalomtaka Wema kuna watu wachache akiwemo Diamond mwenyewe, baba yake, Abdul Jumaa ambaye kwa upande wake alitamka wazi: “Wema ndiye mkwe wa ukweli kabisa.”
Baba huyo alikwenda mbali na kusema anamkubali Wema kwa sababu ana nyota kali na ana roho nzuri hivyo akiendelea kuwa na mwanaye atakuwa na mafanikio tofauti na alivyokuwa na Penny.
Pia ilijulikana kuwa kundi hilo lina mtu mwingine, ndugu wa Diamond aitwaye Rommy Jones ambaye amekuwa akionekana na Wema mara kwa mara hasa wakati msanii huyo akiwa amesafiri.
HALIMA KIMWANA AITWA KIGEUGEU
Taarifa nyingine zilidai kwamba katika sakata hilo, Halima kimwana amekuwa akiitwa kigeugeu kutokana na kutokuwa na upande anaosimamia. “Mara utamuona na Wema ghafla unamuona tena na Penny, yule hata haeleweki. Anajichetua sana,” kilisema chanzo chetu.
MAMA DIAMOND ANASEMAJE?
“Mimi siwezi kumchagulia Diamond mwanamke wa kuwa naye, yeye mwenyewe ataamua kwa sababu ni mtu mzima kwa hiyo siwezi kumpangia au kumchagulia mwanamke wa kuwa naye,” alisema mama Diamond bila kukanusha kuwa na ukaribu zaidi na Penny.
MSIKIE HALIMA KIMWANA
Baada ya kuwatafuta Diamond, Wema na Penny bila mafanikio, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Halima Kimwana ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Sisi tuko karibu na Penny kwa sababu anapenda kujichanganya na sisi hivyo hata Wema akija kutuchukua na kutaka twende naye klabu hatukatai kwa sababu wote ni mawifi zetu.
“Hatubagui kwani hakuna siku ambayo Wema alishataka kuwa na sisi tukamkatalia.”
MASWALI
Hivi karibuni picha za Penny akiwa na mawifi zake kwenye shughuli ya kumtoa mtoto wa ndugu yao zilivuja ambapo ndani ya sherehe hiyo pia Diamond alikuwepo akiwa anacheza dufu lakini Wema hakuonekana, jambo lililozua maswali.
GPL
0 comments: