SERIKALI imeongeza idadi ya askari bungeni baada ya kubainika kuwa kuna njama zimepangwa na kundi la baadhi ya wajumbe kutaka kumzomea Rais Jakaya Kikwete, Tanzania Daima limedokezwa.Habari ambazo gazeti hili limezipata, zilidai kuwa kundi hilo litamzomea Rais Kikwete wakati wa kulihutubia Bunge endapo tu atazungumzia msimamo wa Chama chake Cha Mapinduzi (CCM) wa kutaka serikali mbili na kupingana na maoni ya wananchi waliyoyatoa kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya Jaji Joseph Warioba, wanaopendekeza muundo wa serikali tatu.Ingawa haijajulikana ni kundi gani la wajumbe wanaopanga njama hizo, lakini wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unanyoshewa kidole kwamba ndio wanaohusika na mkakati huo
0 comments: