Baada ya Marekani kuripotiwa kukumbwa na
baridi kali hali iliyopelekea baadhi ya viwanja vya ndege, Barabara na
reli kufungwa kwa muda..headlines zimehamia Taiwan.
Wakati Tanzania ikikadiriwa kuwa na
nyuzi 38°C na kuendelea kwa sasa, unaambiwa mji wa Taipei uliopo Taiwan
umekumbwa na baridi kali huku nyuzi joto ikiwa ni 4°C, joto ambalo ni
dogo na halijawahi kutokea kwa miaka 44 iliyopita.
Mpaka sasa tayari watu 52 wamepoteza
maisha kutokana na kushindwa kuhimili baridi kali…wengi wao wakiwa
wameugua nimonia pamoja na maradhi ya moyo.
Watalii zaidi ya 60,000 pia wamekwama Korea Kusini kutokana na baridi kali, pia safari za ndege zimesimama kwa muda.
Miji mingine iliyoathirika ni Hong Kong na Japan.
0 comments: