Wizara ya Fedha ya
Marekani imeiambia BBC kuwa rais wa Urusi Vladmir Putini anakula
rushwa.Tayari serikali ya Marekani imeshawawekea vikwazo wasaidizi wa
rais Putin na inaonekana ni mara ya kwanza kwa kumhusisha moja kwa moja
rais huyo na rushwa.
Msemaji wa wa rais huyo Urusi ameaiambia BBC hakuna maswali jambo lolote linapaswa kujibiwa kwa sababu ni wa kutunga.Tuhuma hizi zinakuja siku chache ambapo hivi majuzi tume ya uchunguzi ya Uingereza iliyokuwa ikichunguza mauaji ya jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinesko lilimtuhumu pia Putin kuwa huenda alitoa amri ya kuuawa kwa jasusi huyo.
Litvinenko aliyekuwa akifanya kazi katika idara ya usalama ya urusi aliuawa kwa sumu ya polonium mjini London mwaka 2006.
Adam Szubin anayesimamia vikwazo vya Wizara ya fedha vya Marekani amekiambia kipindi cha Palorama cha BBC kuwa rais wa Urusi ni mla rushwa na hilo lilifahamamika na serikali ya Marekani miaka mingi iliyopita.
"Tumemwona akiwaneemesha marafiki zake na watu wake wa karibu na kuwakandamiza wale ambao sio marafiki wake kwa kutumia rasilimali za taifa kama utajiri wa nishati au mikataba baina yao na serikali amekuwa akitoa maagizo iwanufaishe wale ambao anaamini watamnufaisha na kuwatenga wale wasiomnufaisha. Kwangu mimi hiyo hiyo ni sura ya rushwa."
Maafisa wengine wa Marekani waliogoma kuhojiwa kuhusu utajiri anaodaiwa kuwa nao Putin ambaye na Szubin pekee aliyekubali kushiriki kwenye uchuguzi huo uliofanywa na kipindi cha Panorama hata hivyo alikataa kutoa maoni yake kuhusu ripoti ya siri ya Shirika la kijasusi la CIA iliyotolewa mwaka 207 kuhusu utajiri wa Putin unaofikia dola bilion 40.
Mwaka 2008 Putin Mwenyewe alizielezea tuhuma kwamba ni ana utajiri mkubwa kuwa ni propaganda na hazina maana.Kuhusu tuhuma hizi za Rushwa Putin alikataa kuhojiwa na kipindi hicho cha Panorama.
0 comments: