Na.Vero Ignatus Arusha.
Katibu
mkuu baraza la Sanaa Tanzania amewataka wazazi na walezi wa hapa nchini
kuwalea watoto na kuhakikisha kuwa wanaishi katika maadili ili kuzuia
mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa tamasha la kwanza la Tanzania Tukuza Utalii
Genesis 1,Godfrey Ngereza alisema kuwa tanzania imebarikiwa kwa tunu
mbali mbali hivyo watanzania hawana budi kuzitunza na kuzilinda.
Aidha alisema kuwa wazazi hawana budi kuwafundisha watoto uzalendo na kuhakikisha kuwa tamaduni zilizopo haziishi."Waswahili
walisema samaki mkunje Angali mbichi tukiwalea watoto vizuri ni ngumu
kuona maadili yanamomonyoka kwa kuwa tutakuwa tumetengeneza watoto wema"
Alisema Godfrey
Kwa
upande wake Raisi wa Mtandao wa wasanii wa nyimbo za Injili
Tanzania(TAGOANE)Dkt.Godwin Maimu Nnyaka alisema kuwa watoto yatima
hawahitaji mavazi na chakula peke yake bali kujengewa msingi bora wa
maisha yake.
Dkt.Nnyaka alisema wakati umefika wazazi kuwalea watoto katika misingi ya Imara na kuhakikisha wanakuwa wazalendo.Aidha
alisema kuwa kupitia tamasha hilo litasiadia kujenga vijana wenye hofu
ya Mungu na kurejesha uzalendo na maadili kwa vijana.
Nao
baadhi ya Washiriki akiwepo mmiliki wa kituo cha faraja Ophanage Faraja
Maliaki aliishukuru TAGOANE na kuwataka wadau wengine kuungana na
watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kuwapa faraja kwa
kuwa nao wanastahili kuheshimiwa kama watoto wengine.
Katibu
mkuu mtendaji Baraza la sanaa nchini( Basata)Godfrey Mngereza akiwa
anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo.Picha zote kwa Idhini ya
Vero Ignatus Blog
Rais
wa Mtandao wa Wasanii wa wasanii wa Muziki wa Injili Tanzania na
maandili nchini Tanzania (TAGOANE) Dkt.Godwin Maimu akiwa anazungumza
katika ufunguzi wa Tamasha la Tukuza utalii Tanzania lililozinduliwa
rasmi Jijini Arusha.
Baadhi
ya watoto waliokuwa wanaishi katika mazinhira hatarishai na baadae
wakachukuliwa na kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto yatima.Picha
kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Rais
wa Tagoane Dkt.Godwin Maimu akiwa anacheza pamoja na watoto katika
Tamasha lililoandaliwa la Tukuza Utalii Tanzania lililoandaliwa na
Tagoane.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la sanaa nchini (BASATA)
pamoja na Rais wa Tagoane nchini wakikata keki kama ishara ya Ufunguzi
wa Tamasha la Kuza Utalii Tanzania .
Shamrashamra zikiendelea
Watoto
wanaolelewa katika Kituo cha Faraja wakiwa katika picha ya pamoja
wakiwa na mlezi Faraja Maliaki,wapo zaidi ya watoto 200 katika ukubi wa
Club D Jijini Arusha.
Mgeni
rasmi kutoka Baraza la sanaa la Taifa (Basata)Godrey Mngereza akifurahi
pamoja na watoto yatima katika tamasha lililoandaliwa na Tagoane Jiiini
Arusha.
Wakila chakula pamoja na watoto katika Tamasha
Meza
kuu Rais wa Tagoane,Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la Sanaa nchini
(Basata)Katibu mkuu Tagoane,na wakurugenzi wa vituo vya kulelea watoto
yatima Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Muimbaji
wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar es salaam Gifted Wilson akiimba
katika uzinduzi wa tamasha la Tukuza Utalii Tanzania Genesis 1 Jijini
Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Muimbaji wa nyimbo za Injili Miriam Makunja kutoka Arusha akiimba. Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Muimbaji Wolter Chilambo kutoka Jijini Dar es salaam akiwa anaimba katika Tamasha hilo.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Hellen Masai akutoka Arusha kiimba .Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Katibu
mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifa akiwa anafurahia kwenye ufunguzi
wa Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania likilofanyika Jijini Arusha.Picha
kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Katibu
mkuu mtendaji wa Baraza la sanaa Nchini (Basata)wa kwanza kushoto akiwa
pamoja na Rais wa Tagoane katika uzinduzi wa Tamasha la Tukuza Utalii
Tanzania.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Watoto
wakionyesha mavazi ya ubunifu chini ya Mwanamitindo mbunifu Diana
Magesa kutoka Mwanza,Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Picha
za watoto yatima waliohudhuria katika tamasha la Tukuza Utalii Genesis 1
lililofanyika Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
0 comments: