Monday, 2 June 2014

SAMUEL ETO`O AFUNGA NA KUSHANGILIA KWA STAILI YA KIBABU KINACHOTEMBELEA MKONGOJO, AENDELEA KUMPIGA MADONGO MOURINHO


Opener: Samuel Eto'o pokes the ball home to give Cameroon the lead against Germany on Sunday night
Hitting back: Eto'o repeated this 'old man' celebration for Cameroon in response to Jose Mourinho's jibes about his age
Hitting back: Eto'o repeated this 'old man' celebration for Cameroon in response to Jose Mourinho's jibes about his age
 Eto’o amerudia tena staili ya kuonesha uzee wake baada ya kufunga bao na haya bado ni majibu kwa Mourinho.

MSHAMBULIAJI mkongwe, Samuel Eto`o jana usiku aliifungia bao la kuongoza timu ya taifa ya Cameroon katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kujiandaa na fainali za kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 2-2, mkongwe huyo mwenye miaka 33 alifunga bao dakika ya 62 na kushangilia kwa `staili` yake ya kikongwe anayetembelea mkongojo.
Ikumbukwe aliwahi kushangilia kwa  `staili` hiyo wakati alipoifungia Chelsea bao ikiwa ni kejeli kwa kocha wake, Jose Mourinho aliyekuwa anambeza kuwa kwasasa Mcameroon huyo amezeeka.
Eto’o, aliingia katika vita ya maneno baada ya maneno hayo ya kejeli kutoka kwa Mourinho aliyehoji umri wake sahihi mapema mwanzoni mwa msimu, na baada ya kufunga jana alikimbilia sehemu ya kibendera cha kona na kushangilia kwa staili yake ya comedi inayoonesha uzee wake.
Kikosi cha Ujerumani: Weidenfeller, Boateng, Mertesacker, Hummels, Durm (Howedes, 85), Khedira (Kramer, 73), Kroos, Muller, Ozil (Podolski, 63), Reus, Gotze (Schurrle, 58).
Wachezaji wa akiba: Zieler, Grosskreutz, Schmelzer, Schweinsteiger, Klose, Mustafi, Draxler, Ginter, Volland.
Wafungaji wa magoli: Muller, 66, Schurrle, 71.
Aleyoneshwa kadi ya njano: Boateng. Kikosi cha Cameroon: Itandje, Djeugoue, Bedimo (Assou-Ekotto, 58), N’Koulou, Song, Mbia (N’Guemo, 46), Enoh, Matip, Choupo-Moting, Moukandjo, Eto’o (Webo, 90).

Wachezaji wa akiba: N’Djock, Kana Biyik, Nounkeu, Aboubakar, Makoun, Chedjou, Idrissou, Bong Songo, Nyom, Salli, Olinga, Loe.
Wafungaji wa magoli: Eto’o 62, Choupo-Moting, 78.
Aliyeoneshwa kadi ya njano: Song, Enoh.
Mwamuzi: Damir Skomina (Slovenia)
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Inter alifunga bao la kwanza lakini dakika chache baadaye Thomas Muller aliunganisha krosi nzuri ya Jerome Boateng na kusawazisha bao hilo.
Wenyeji waliandika bao la kuongoza kupitia kwa nyota wa Chelsea Andre Schurrle baada ya kutumia vyema pasi ya Lukas Podolski.
Hata hivyo bao hilo halikudumu baada ya  Eric Maxim Choupo-Moting -kuisawazishia Cameroon.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: