Inspector Henry akiwasihi
mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti
wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya
taratibu za kesi.
*********
Matukio ya ajabu yanayofanywa na mahabusu wanaoshinikiza kesi zao
kusikilizwa haraka ikiwa ni mbinu wanazoamini zitasaidia katika kile
wanachoeleza kuwa ni kudai haki zao yanaendelea kuonekana ambapo jana
mahabusu jijini Mwanza walifanya tukio la aina yake.
Mahabusu wawili kati ya sita wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji jana
walijaribu kutoroka kutoka kwenye mstari wa utaratibu wa kuingia
mahakamani na kisha kung’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku
mmoja wao akivua nguo zote na kubaki mtupu.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi katika Mahakama ya
Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.
Thobias Warioba, mmoja kati ya mahabusu hao ndiye aliyevua nguo zote
na kubaki mtupu na kisha kupiga kelele akiwa ameshikilia mlingoti
akieleza kilio chake.
“Haiwezekani tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu
hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiwa kesi.
"Tunaomba haki zetu, polisi wanatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu mwaka 2011tulipokamatwa.
"Tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe.” Alisema Thobias Warioba.
"Tunaomba haki zetu, polisi wanatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu mwaka 2011tulipokamatwa.
"Tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe.” Alisema Thobias Warioba.
Inspector wa polisi alijitambulisha kwa jina la Henry aliwataka
watuhumiwa hao waondoke katika mlingoti na kuvaa nguo ili waingie
mahakamani kwani kitendo walichokuwa wakikkifanya ni kosa la jinai..
“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili
ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vyema mkaondoka kwenye mlingoti huu
na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa.”
Alisema Inspecta Henry.
Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji
Inspector Henry (shati la
bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za
Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa
ameng’ang’ania mlingoti wa Bendera ya Taifa
Ushawishi ukiendelea
Mahabusu Thobiasi Warioba
(aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu
waking’ang’ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza
kuzungumza na waandishi wa Habari.
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
Mashuhuda
0 comments: