Monday, 2 June 2014

Video: Mbwa asababisha ndege kutua ghafla Kansas City, Marekani

Ndege ya shirika la Marekani lililazimika kuchukua tahadhari na kutua baada ya mbwa wa ulinzi kuachia kinyesi mara kwa mara katikati ya siti za abiria.
Andrew Christie, mzungumzaji wa shirika hilo, alisema safari hiyo kutoka Los Angeles kwenda Philadelphia ilisitishwa kwenye kituo cha mji wa Kansas.
Hatimaye timu ya usafi iliwasili kwenye eneo la tukio hilo, ila safari ya abiria hao iliongezeka muda mara mbili na kuwa zaidi ya saa 14.
Safari ya ndege hiyo iliendelea baada ya uchafu huo kusafishwa na wafanyakazi wa ndege hiyo ya Marekani.
Abiria na mbwa wake walihamishiwa kwenye ndege nyingine.
Bwana Christie alisema tukio hilo ni la “nadra na hutokea kwa bahati mbaya.”
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: