HUYU HAPA NDO MBADALA WA PWEZA KATABIRI BRAZILI ITASHINDA CHECK VIDEO YA KOBE MTABIRI
Wakati fainali za kombe la dunia zikianza kesho nchini Brazil, mashabiki wa soka nchini Brazil kwa kuipa nafasi kubwa timu yao ya taifa kufanya vyema katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia uliopangwa kuchezwa Arena de São Paulo huko mjini São Paulo.
Mmoja wa mashabiki wa soka nchini Brazil ameibuka na harakati za ubashiri kwa kutumia kasa huku akikumbushia katika fainali za mwaka 2010 ambapo ubashiri wa michezo kadhaa ya fainali hizo ulimuhusisha Pweza Paulo.
Kasa huyo aliebatizwa jina la The Loggerhead Turtle, *Big Head*, amebashiri mchezo huo wa ufunguzi akiwa katika bwawa la kuogelea ambapo kigezo kikubwa kinachotumika anawekewa samaki kwenye pande mbili zilizo na bendera za nchi zinazoshinda.
Ubashiri wa kiumbe huyo unaaminiwa pale anapochagua kula samaki wa upande wenye bedera ya nchi fulani ambapo inaaminika upande huo ndio utakaoibuka na ushind
0 comments: