Hali bado sio shwari kwa upande wa Rais wa FIFA, Sepp Blatter…
Zimepita siku chache tu tangu atangaze kwamba ataachia ngazi kwenye
uongozi wa taasisi hiyo kubwa ya soka duniani kutokana tuhuma za rushwa
kuiandama taasisi hiyo.
Leo hii zimetoka taarifa nyingine ambazo
zimeibua tetesi za siku nyingi kwamba Rais huyo wa FIFA alikuwa hana
uhusiano mzuri na mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo.
Gazeti lenye heshima ndani ya Spain, El Mundo limeripoti kwamba aliyekuwa mchumba wa Ronaldo, Irina Shayk alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Sepp Blatter katika vipindi viwili tofauti.
El Mundo linaripoti kwamba Blatter alikuwa na uhusiano muda mrefu na Mrembo huyo wa kirusi baada ya kuachana na mcheza tennis Ilona Boguska lakini hiyo ilikuwa ni kabla ya kukutana na mwanamama Linda Barras.
Habari hiyo ya Irina na Blatter imeandikwa kwenye na mwandishi wa gazeti la El Mundo, Rosalia Sanchez amesema kwamba taarifa hiyo ya siri ya mahusiano ya Irina na Mzee Blatter ilipata
kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika wakati anafanya uchunguzi wa
taarifa za rushwa na mahusiano zinamhusu boss huyo wa FIFA.
Uhusiano wao inasemekana ulianza mwaka 2002, wakatengana na kuja kuendelea tena mwaka 2014, wakati Irina akiwa bado na uhusiano na Cristiano Ronaldo ambaye walianza mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa mwaka huu walipotangaza kuachana.
Taarifa ya uhusiano ya Blatter na Irina
pia imeripotiwa katika vyombo vya habari vya nchi za Peru, Portugal,
Mexico na Vietnam pamoja na kuvuta wmijadala ya watu wengi kwenye
mitandao ya kijamii.
Msemaji wa Irina Shayk kaulizwa juu ya tuhuma hizi ila hakujibu chochote..
0 comments: