Thursday, 5 June 2014

Cristiano Ronaldo ‘arogwa’ na mganga kutoka Ghana

Mganga Kwaku Bonsam kutoka Ghana ameibuka na kudai kuhusika na majeraha yanayomwandama Mreno Cristiano Ronaldo.
Mganga Nana Kwaku Bonsam kutoka Ghana ameibuka na kudai kuhusika na majeraha yanayomwandama nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo.
Nyota huyo wa Real Madrid anasumbuliwa na matatizo ya misuli na kumfanya akose mechi za kirafiki a Kombe la Dunia dhidi ya Mexico na Ireland, Mganga Nana Kwaku Bonsam amedai anahusika na matatizo ya mshindi huyo wa Ballon d’Or, akidai kuwa ni tatizo la kiroho.
“Najua majeraha ya Cristiano Roanaldo yanasababishwa na nini, na nalifanyia kazi hilo”, mganga huyo alikiambia kituo cha redio cha Ghana cha Angel FM.
“Sitanii kuhusiana na hili. Wiki iliyopita, nilitafuta mbwa wanne na kuwatumia kutengeneza roho maalumu inayoitwa “Kahwiri Kapam’.
“Miezi minne iliyopita nilisema kuwa nitashumghulikia Cristiano Ronaldo na kumfanya asicheze Kombe la Dunia au asicheze mechi dhidi ya Ghana na jambo lingine zuri ni kumfanya apone majeraha yake”, aliongeza mganga huyo.
“Kamwe hawezi kutibiwa na daktari, maana hatoweza kupona kwani chanzo cha majeraha yake ni tatizo la kiroho. Leo ni kwenye goti lake, kesho ni paja, kesho kutwa ni tatizo jingine”.
Ghana watacheza na Ureno Juni 26 mjini Brasilia, ambapo itakuwa ni mechi za mwisho ya Kundi G, ambalo linahusisha timu ya Ujerumani na Marekani.

post written by:

Related Posts

0 comments: