Home
Sports
BONANZA LA 9 WANAHABARI KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA JUNI 28 JIJINI ARUSHA
BONANZA LA 9 WANAHABARI KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA JUNI 28 JIJINI ARUSHA
in
Sports
published on 00:09:00
Arusha.Bonanza la waandishi wa habari na watangazaji Kanda ya Kaskazini
linatarajiwa kufanyika june 28 katika viwanja vya General tyre jijini
Arusha na kushirikisha zaidi na wanahabari 150 na wadau wa habari.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Arusha , Katibu wa chama cha waandishi
wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa
Juma, alisema maandalizi muhimu ya Bonanza yameanza.
Juma
alisema bonanza hilo,ambalo huandaliwa na TASWA Arusha na kampuni ya MS
UniquePromotion litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari wa
michezo mkoa wa Arusha, ambayo itashirikisha baadhi ya wajumbe wa
kamati ya tendaji ya TASWA Taifa.
Hata
hivyo alisema bado TASWA Arusha na kampuni ya MS Unique wanatafuta
wadhamini wa bonanza hilo ambalo litakuwa ni la tisa kufanyika.
Juma alisema hivi karibuni wadhamini wa bonanza hilo, watatangazwa sambamba na zawadi kwa washindi.
Alisema
katika tamasha hilo, wanahabari na wadau wa habari watashiriki katika
michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia,mpira wa pete, kukimbiza
kuku na kucheza muziki.
Katika
tamasha la mwaka jana, hakukuwa na bingwa wa soka baada ya TASWA Dar es
Salaam na timu ya chuo cha Uandishi wa habari(AJTC) kushindwa kufungana
na kuamua kugawana sehemu ya zawadi iliyokuwa imepangwa.
Kwa
upande wa mpira wa pete TASWA Dar es Salaam, alishinda, huku katika
mchezo wa kukimbiza kuku TASWA Arusha ilishinda na katika kamba timu ya
Sunrise ilishinda wakati timu ya radio 5 na Arusha one zilitamba katika
mbio za magunia.
Timu
ya Waandishi na watangazaji toka mkoa wa Manyara ya ORS ilishinda
zawadi ya timu yenye nidhamu,timu nyingine zilizoshiriki ni Wazee
Klabu,Pespi,TBL na timu ya Kitambi noma.
0 comments: