Chama cha Chansela
wa Ujerumani Angela Merkel kimeshindwa katika uchaguzi wa majimbo,
matokeo ya utafiti wa baada ya uchaguzi yanaonesha.
Matokeo hayo
yanaonesha chama cha Christian Democrats kimeshindwa katika majimbo ya
Baden-Wuerttemberg naRhineland Palatinate, lakini bado kimeendelea
kutawala Saxony-Anhalt.Chama cha AfD kinachowapinga wahamiaji, kimeimarika pakubwa katika majimbo yote matatu.
Uchaguzi huo ulitazamwa na wengi kama kigezo cha uungwaji mkono wa sera ya Chansela Merkel ya kuwapokea wakimbizi.
Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni moja waliingia Ujerumani mwaka 2015.
Naibu Chansela wa Ujerumani alisema Jumamosi kwamba kuimarika kwa AfD hakutabadili sera za serikali yake kuhusu uhamiaji.
“Huu ni msimamo wazi ambao tutaendelea kuutetea, wa kutetea utu na ubinadamu. Hatutabadili msimamo wetu sasa.”
Lakini mjini Berlin Jumamosi, karibu waandamanaji 2,000 wa mrengo wa kulia walibeba bendera za Ujerumani na kuimba "Merkel sharti aondoke!" na "Sisi ndio watu!"
Pigo hilo kwa Chansela Merkel limetokea siku chache kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Ulaya wa kukamilisha mkataba kati ya EU na Uturuki wa kudhibiti kuingia kwa wahamiaji na wakimbizi.
Mkataba huo, ambao utapelekea wahamiaji wanaowasili nchini Ugiriki wakirejeshwa Uturuki, unakabiliwa na changamoto za kisheria na kisiasa.
Wanasheria wanajizatiti kutafuta mpango ambao utatimiza masharti ya kimataifa kuhusu wakimbizi.
Umoja wa Mataifa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu wametaja mpango huo kuwa usiofuata maadili na haramu.
0 comments: