Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa
amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) , amefanya
uhakiki wa madeni yanayodaiwa serikali na watumishi na kubaini madudu
kibao.
Amesema
madai mengine yameonyesha mashaka ambapo amewataka wakurugenzi wa
Halmashauri na Wakaguzi wakuu wa ndani kujiridhisha ukweli wa madai hayo
kabla ya kuyafikisha serikalini kwa ajili ya malipo.
“Madai
mengine yanatia mashaka, sisi hatuhitaji kuletewa madeni ya hovyo hovyo
ni vema Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wa ndani wakajiridhisha
kabla kuyapeleka serikalini kwa ajili ya malipo.
"Madeni
mengine ya ajabu, mfano unakuta mtumishi mmoja anaidai serikali sh.
milioni 30, jambo ambalo ni gumu hata kama alihamishwa haiwezekani
kufikia kiwango hicho, pia kuna baadhi ya majina yamejirudia mara nne,” amesema.
Waziri
Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa
hospitali ya wilaya ya Ruangwa alipotembelea Hospitali hiyo wakati akiwa
katika ziara ya kikazi iliyolenga kukabidhi msaada wa vifaa tiba
alivyovitoa kwa ajili ya hospitali hiyo.
Amesema
kuwa serikali italipa madeni yote inayodaiwa baada ya kumaliza
kuyafanyia uhakiki, hivyo aliwaomba watumishi kuwa na subira wakati
serikali ikiendelea zoezi la kuyahakiki ili kuweza kulipa deni sahihi
inalodaiwa.
Awali
akisoma taarifa ya Idara ya afya kwa Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa
Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk. Japhet Simeo amesema idara ya afya
inakabiliwa na madeni ya watumishi ambayo ni sh. milioni 109,662,483.
Amesema
madeni hayo yametokana na likizo, matibabu, uhamisho wa ndani na nje ya
wilaya, gharama za mizigo kwa watumishi waliostaafu, ambapo
halmashauri imejipangia utaratibu wa kulipa madeni hayo pindi inapotokea
fedha kutoka serikali kuu.
Hata
hivyo kasi ya mtiririko wa fedha ni ndogo ukilinganisha na mahitaji
halisi ya maslahi ya watumishi ambapo Halmashauri inawapongeza na
kuwapongeza watumishi wa Idara ya afya kwa kuendelea kuwa wavumilivu na
kuwahudumia wananchi.
Dk.
Simeo amesema halmashauri inawapongeza Rais Dk. John Magufuli na Waziri
Mkuu, Majaliwa kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuongeza mapato nchini,
ambapo wana matumaini kuwa watumishi wataboreshewa maslahi na stahiki
zao ili kuchochea motisha kiutendaji.
Katika
hatua nyingine Dk. Simeo alizungumzia upatikanaji wa dawa, alisema
ambao umeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka jana na kufikia asilimia 80
mwaka huu dawa muhimu katika vituo vyote vya kutolea huduma ambavyo viko
32.
0 comments: