Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli amesema
amewatuma watu kuwarekodi mawaziri ambao wamesikika wakilalamika
'chinichini' kukatwa kwa fedha za matumizi mengineyo ( OC- Other Charges
) katika bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha.
"Mawaziri
wengine nasikia wanalalamika kweli,sasa nimetuma watu kuwarekodi kwa
sababu mind set (fikra) zao bado hazijabadilika,wanafikiri watu bado
tupo kwenye trend hiyo hiyo,wasomi ni wengi,unaweza ukawateua leo na kesho ukawabadilisha, ili mradi twende kwenye trend ninayoitaka," alisema Magufuli.
Rais
Magufuli aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati
akizungumzia hatua ya bunge kubana matumizi na kuwezesha kupatikana kwa
kiasi cha shilingi bilioni 6 ambazo zitaelekezwa kwenye utengenezaji wa
madawati.
“Chief Secretary(Katibu Mkuu Kiongozi ), huo ndio muelekeo kwa Makatibu Wakuu, waache kudai OC… Nawasikia watu wanadai eti OC ni kidogo. Wakiona hazitoshi basi waache kazi, maana wenzao wabunge wamesema ni nyingi na wamebana matumizi," alisema Rais Magufuli na kuongeza:
"Katibu
wa bunge ameonyesha mfano,kwa nini wengine washindwe? Mtaona katika
bajeti tumekata hizo OC ambazo zilikuwa ni ulaji mtupu, tumeongeza
bajeti ya maendeleo kutoka kati ya bilioni 26 na 27 hivi za mwaka jana
hadi asilimia 40, fedha za bajeti ziende kufanya miradi ya maendeleo,
zikawasaidie watu masikini."
0 comments: