Wimbo wa mapenzi
wa mwanamuziki wa Uingereza Ed Sheeran unaongoza kwa kupendwa sana na
watu kama wimbo wa kufungua jukwaa wakati wa harusi.
Kwa mujibu wa
mtandao wa Spotify, ambao wamechunguza maelfu ya orodha ya nyimbo
zinazosambazwa zaidi katika mtandao huo, wimbo wa Thinking Out Loud
unaongoza.Wimbo wa At Last wake Etta James ni wa pili nao wimbo wa Ray LaMontagne, You Are the Best Thing ni wa tatu.
Nyimbo nyingine maarufu zilizo kwenye orodha ya 50 bora duniani ni wimbo wake Frank Sinatra uitwao The Way You Look Tonight na wimbo wa Marry You wake Bruno Mars.
Nyimbo kumi zinazopendwa zaidi duniani kwa mujibu wa Spotify, mtandao unaowawezesha watu kusikiliza nyimbo moja kwa moja mtandaoni, ni:
- Thinking Out Loud - Ed Sheeran
- At Last - Etta James
- You Are the Best Thing - Ray LaMontagne
- All of Me - John Legend
- A Thousand Years - Christina Perri
- Make You Feel My Love - Adele
- I Won’t Give Up - Jason Mraz
- Everything - Michael Bublé
- Better Together - Jack Johnson
- Amazed - Lonestar
0 comments: