Saturday, 26 April 2014

KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU, THE REAPERS WAMEREJEA TENA

Baadhi ya waimbaji wa The Reapers wakiwa kazini.
Baada ya kimya cha mda mrefu hatimaye kwaya ya The Reapers kutoka Kanisa la Pentekoste Kimara jijini Dar es salaam, ambao wametamba na album ya 'Ninaye Rafiki' wameachia nyimbo mpya zilizobebwa na wimbo 'Wanipa Raha' huku pia wanatarajia kurekodi DVD live ya nyimbo hizo katika kanisa la Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) kwa mchungaji Huruma Nkone mnamo tarehe 25 mwezi ujao.
Akizungumza na GK mmoja wa viongozi na mwalimu wa kwaya hiyo bwana Moses Fumbuka amesema kwasasa kwaya hiyo iko kwenye mazoezi mazito kwaajili ya tukio hilo ambalo pia litawajumuisha waimbaji wao wote waliosolo ama kuanzisha nyimbo katika album iliyopita ya 'Ninaye Rafiki' lakini pia watu watarajie waimbaji wapya waliojiunga na kwaya hiyo.

Sikiliza wimbo wao mpya hapa kwa hisani ya

Fumbuka amesema wameamua kurekodi picha za moja kwa moja wakiimba kutokana na kwamba
nyimbo walizonazo haipendezi kuziimba kwa maigizo hivyo wameona ni bora kurekodi pale ili watu watakaofika wakakutane na Mungu moja kwa moja lakini pia kuna uzuri wake wakurekodi kanda ya namna hiyo. The Reapers ama wavunaji wametokea kuvuma sana ndani na nje ya nchi kutokana na kazi nzuri ya Ninaye Rafiki ambayo imebeba nyimbo zilizotokea kupendwa na wengi kama vile Haja ya moyo, Tanzania, Nakuhitaji Roho na nyinginezo.
Kazi kwako mkazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake weka kwenye ratiba yako kuanzia sasa kwamba tarehe 25/5/2014 ni siku ambayo kwaya ya The Reapers watakuwa wakirekodi DVD yao ya kwanza live katika kanisa la VCCT kwa mchungaji Huruma Nkone lililopo mitaa ya Mbezi beach jijini Dar es salaam. Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea GK tutakuwa tukikufahamisha yanayojiri kuiendea siku hiyo muhimu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: