Siku
ya Jumapili, tarehe 20 Machi 2016, Zanzibar itashuhudia, kwa mara
nyingine tena, ubakwaji wa demokrasia kwa kufanyika kile kinachoitwa
Uchaguzi wa Marudio’ kufuatia tamko binafsi la Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alilolitoa tarehe
28/10/2015 kwamba ameufuta Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25/10/2015 na matokeo
yake yote.
Tangazo hilo la Jecha Salim Jecha, lililo kinyume na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984 na linalopingana na Katiba ya Zanzibar, lilikuja baada ya waangalizi wote wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Madola (The Common Wealth), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na Waangalizi wa Marekani na Uingereza, kutoa taarifa zao na kueleza kuridhishwa na mwenendo wa Uchaguzi huo na kwamba ulikuwa huru na wa haki kwa sababu ulifuata taratibu za kisheria na ulifanyika kwa amani.
Aidha,
baada ya kukamilika kwa hatua ya upigaji kura, wadau na washiriki wa
ndani wa uchaguzi huo akiwemo, yeye mwenyewe, Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar, mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dk. Ali
Mohamed Shein, mgombea wa Urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na
wagombea kutoka vyama vyengine walikiri kwamba uchaguzi ulikuwa huru na
wa haki.
Ghafla,
kutokana na shindikizo kubwa kutoka kwa viongozi wa Chama chake,
ambacho aliwahi kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge kupitia chama hicho na
kuanguka katika hatua ya kura za maoni, Mwenyekiti wa Tume alitangaza
kuufuta Uchaguzi huo kwa kutumia hoja na maelezo yaliyotolewa na CCM
baada ya kubaini imeshindwa kwenye nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Tokea
kutolewa kwa tangazo hilo kumekuwepo na juhudi mbalimbali ndani na nje
ya nchi za kutafuta suluhisho kutokana na mgogoro ulioibuliwa kwa
makusudi kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi CCM kuondokana na
aibu ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 25 Oktoba 2015.
Miongoni
mwa juhudi za ndani ni pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF,
Maalim Seif Sharif Hamad, kukutana na viongozi mbalimbali akiwemo
mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dr. Ali Mohamed Shein, Marais
wastaafu wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John
Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ili kufanya
mazungumzo na kuiepusha nchi kutokana na migogoro na mifarakano ya baada
ya uchaguzi. Viongozi wa dini mbalimbali nao pia walichukua dhamana na
dhima ya kuhakikisha kuwa mgogoro wa Zanzibar unapatiwa ufumbuzi kwa
lengo la kuibakisha Zanzibar katika hali ya umoja na masikilizano
miongoni mwa wananchi wake.
Kwa
upande wa juhudi za nje, jumuiya ya kimataifa imesikika mara kadhaa
ikitoa matamko na kuchukua hatua mbalimbali kuitaka Tume ya Uchaguzi
kukamilisha kazi ya uhakiki na majumuisho ya matokeo ya uchaguzi na
kumtangaza mshindi.
Jumuiya
hiyo pia iliushauri uongozi wa vyama vya CCM na CUF kukaa pamoja
kuzungumza jinsi ya uundwaji na uendeshaji wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Zanzibar kama yalivyo matakwa ya Katiba ya Zanzibar na
kuhakikisha kuwa demokrasia, haki za binadamu na amani vinaenziwa,
kulindwa na kutunzwa.
Kwa makusudi na kwa lengo maalum, hatua zote hizo zimepuuzwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Serikali zote mbili, na hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar alitangaza kufanyika kwa kile kinachoitwa Uchaguzi wa Marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi 2016.
Kwa makusudi na kwa lengo maalum, hatua zote hizo zimepuuzwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Serikali zote mbili, na hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar alitangaza kufanyika kwa kile kinachoitwa Uchaguzi wa Marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi 2016.
Kupuuzwa
huko kwa juhudi za ndani na nje, kunakochochewa na baadhi ya viongozi
waandamizi wa CCM na Serikali zote mbili, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa
la The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) lililokutana katika
kikao cha dharura tarehe 07 Novemba, 2015, mjini Zanzibar kuzungumzia
hali ya kisiasa hapa nchini kufuatia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba,
2015 lilifikia maamuzi ya kuitaka Tume ya Uchaguzi, pamoja na mambo
mengine, irudi kukamilisha hatua zilizobaki za uhakiki na majumuisho ya
matokeo ya Uchaguzi.
Kimsingi,
Baraza Kuu lilisisitiza halitakubaliana, kwa namna yoyote ile, na hatua
ya kufanya Uchaguzi wa marudio kwa kuzingatia kukosekana kwa uhalali wa
kisheria katika ufutwaji wa matokeo ya Uchaguzi na kwamba uchaguzi
ulishafanyika na kazi ya kuhesabu kura kumalizika.
Tokea
kutolewa kwa tamko la kufutwa kwa Uchaguzi, kutangazwa kwa Uchaguzi wa
marudio, na kutolewa kwa Azimio la Baraza Kuu la Uongozi la CUF,
Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejikuta katika taharuki na
wasiwasi mkubwa na kupelekea khofu isiyomithilika kuhusiana na hali ya
kisiasa na kiusalama ya Zanzibar.
Kwa mfano, kumeripotiwa matukio mengi ya uvunjwaji wa haki za binadamu ambapo raia wasio na hatia wanapigwa na kujeruhiwa vibaya, nyumba na makaazi ya watu kuvunjwa na kuchomwa moto, maeneo ya vyama vya siasa, kama vile barza za CUF, yamehujumiwa kwa kuchomwa moto na ofisi zake kuvunjwa na kuibiwa mali zote kabla ya kuwashwa moto na kuteketea kabisa.
Kwa mfano, kumeripotiwa matukio mengi ya uvunjwaji wa haki za binadamu ambapo raia wasio na hatia wanapigwa na kujeruhiwa vibaya, nyumba na makaazi ya watu kuvunjwa na kuchomwa moto, maeneo ya vyama vya siasa, kama vile barza za CUF, yamehujumiwa kwa kuchomwa moto na ofisi zake kuvunjwa na kuibiwa mali zote kabla ya kuwashwa moto na kuteketea kabisa.
Kwa
mfano, siku ya Jumatatu, tarehe 15, Machi 2016, makundi ya askari
wakiwa na silaha za moto walivamia ofisi ya Chama Cha Wananchi CUF
iliyopo katika eneo la Mpendae na kuvunja na kuiba vifaa mbalimbali vya
ofisi hiyo zikiwemo kompyuta, printers na photocopy machines.
Katika
tukio hilo, maharamia hao walivunja eneo linalotumika kuhifadhia vifaa
vya muziki na kuiba vifaa vyote vya BRASS BAND ya CUF.
Mengi
ya matukio haya yamefanywa na kikundi kidogo cha askari wa vikosi vya
SMZ, ambacho hutumia magari yenye namba za usajili za SMZ na silaha za
moto na kujifunika nyuso zao kwa staili ya ninja kilichoandaliwa maalum
kwa ajili ya kuwahujumu raia, wakisaidiwa na vyombo vya Ulinzi na
Usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sambamba
na hujuma hizi kumeibuka mtindo wa kuwatisha raia kwa kuwavamia
kuwapiga na kuwabambikizia kesi kwa lengo la kuwashikilia katika vituo
vya Polisi, kinyume na utaratibu wa kisheria, na kuwadhalilisha kwa
kuwapiga na kuwatolea maneno ya vitisho na matusi.
Katika
uvamizi uliofanywa katika ofisi ya CUF ya Mpendae, zaidi ya vijana 30
walikamatwa na jeshi la Polisi, lililoshiriki katika uhalifu huo kwa
lengo la kuwapatia ulinzi maharamia waliopewa kazi ya kuhujumu ofisi
hiyo, na kuwarundika katika vituo vya Polisi na kuwanyima dhamana.
Mkakati
wa kuwatisha raia ulielekezwa pia kwa viongozi wa CUF. Tarehe 16 Machi
2016, Jeshi la Polisi lilivamia nyumbani kwake na kumkamata Kaimu
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Mheshimiwa Hamad
Masoud na kumuweka ndani na kumnyima dhamana.
Tukio
hili la kukamatwa Mheshimiwa Hamad Masoud linafuatia kuwekwa ndani na
kunyimwa dhamana kwa aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni inayojulikana
kama Timu ya Ushindi ya Chama Cha Wananchi (CUF) ndugu Mohamed Ahmed
Sultan Al-Mugheir (Eddy Riyami) tarehe 16, Februari 2016 na kuitwa
Polisi Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui tarehe 3
Machi, 2016 kwa kuwataka wanachi wajilinde kutokana na kushamiri kwa
vitendo vya hujuma dhidi ya wafuasi wa vyama vya upinzani vinavyofanywa
na makundi tuliyoyataja.
Vilevile,
jana tarehe 17 Machi, 2016 aliyekuwa Mjumbe katika Timu ya Ushindi ya
CUF na Mgombea Uwakilishi wa jimbo la Chukwani, Mheshimiwa Mansour
Yussuf Himid, aliitwa na Jeshi la Polisi kwa madhumuni ya kuhojiwa.
Sambamba
na haya, kumekuwepo na juhudi kubwa zinazoongozwa na Mamlaka mbalimbali
ikiwemo Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kuvishurutisha vyama vya siasa, hasa vile vilivyotangaza waziwazi
kugomea Uchaguzi wa marudio, kushiriki katika uchaguzi huo kwa lengo la
kuhalalisha mkakati ulioandaliwa wa kulazimisha ushindi wa CCM ambao
waliukosa katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015.
Kwa
mfano, tarehe 25 Januari, 2016, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
iliwasilisha Makao Makuu ya CUF barua yenye kumbukumbu
TUZ/78/16/2015/2016/Vol.I/2 kwa lengo la kutoa taarifa kuhusu uchaguzi
wa marudio.
Kutokana
na barua hii, CUF, kupitia Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Nassor Ahmed
Mazrui, iliiandikia Tume barua yenye kumbukumbu namba
CUF/HQ/AKM/ZEC/037/016/055 ya tarehe 05/02/2016 kujibu barua ya Tume ya
tarehe 4 August, 2015 yenye kumbukumbu TUZ/78/2015/2016/VOL.VI/68 na
barua ya kukumbushia barua yake ya tarehe 17, August, 2015 yenye
kumbukumbu CUF/HQ/AKM/ZEC/037/015/032.
Kwa
barua yake ya tarehe 5 Februari, 2016 CUF iliitaarifu Tume ya Uchaguzi
juu ya maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kutoshiriki katika
Uchaguzi ambao umetangazwa kufanyika tarehe 20/03/2016 kwa sababu
kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 ni batili na kwa hivyo
marudio ya uchaguzi wa tarehe 20 Machi 2016 ni batili pia, na ni kinyume
na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya 1984.
Aidha,
kwa barua hiyo, CUF iliitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kutokana na
Azimio la Baraza Kuu la Uongozi, kuondoa majina ya wagombea wake wote,
akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad, katika orodha ya wagombea wa Uchaguzi
huo na vile vile yasiingizwe katika karatasi za kura kwa uchaguzi wa
marudio.
Zaidi,
tarehe 8 Februari, 2016 Naibu Katibu Mkuu wa CUF aliwasilisha barua,
kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, iliyokuwa na lengo la kuelezea msimamo wa
CUF kuhusiana na kufutwa isivyo halali kwa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba
2015 na kuitishwa kwa kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20
Machi, 2016.
Kwa
barua hiyo pia, CUF ilibainisha mapungufu ya kisheria na ukiukwaji wa
Katiba ya Zanzibar katika tangazo la kufutwa kwa uchaguzi na kwa hivyo
kutothibitisha mgombea yoyote katika ngazi zote za uchaguzi wa zanzibar
kama ilivyotakiwa kufanya na Tume ya Uchaguzi.
CUF
iliikumbusha Tume na kusisitiza juu ya uamuzi wake wa kuitaka tume
kuhakikisha haitumii jina, alama, wala picha ya mgombea yoyote kupitia
CUF katika karatasi za kura.
Hata
baada ya rundo la barua hizi za CUF, zenye lugha rahisi na maelezo
yanayojitosheleza, kwa Tume ya Uchaguzi kukataa kushiriki katika batili
iliyopachikwa jina la uchaguzi wa marudio, tarehe 29 Februari 2016, Tume
ya Uchaguzi, kwa mara nyingine tena, iliiandikia CUF barua yenye
kumbukumbu namba TUZ/78/16/015/016/VOL. I/200 kuitaka CUF kuwasilisha
majina ya mawakala wake katika uchaguzi ambao kimsingi walishautolea
msimamo.
CUF
kwa upande wake ilimwandikia Mkurugenzi wa uchaguzi barua yenye
kumbukumbu CUF/HQ/AKM/ZEC/037/016/056 ya tarehe 03 Machi 2016
kukumbushia msimamo wake wa kutoshiriki Uchaguzi huo na kwamba kutokana
na uchaguzi huo kukosa uhalali kisheria na kikatiba, haioni haja ya
kuwasilisha majina ya waangalizi kwa uchaguzi huo.
Kwa
mara nyingine tena, tarehe 8 Machi 2016, Tume iliiandikia CUF barua
yenye kumbukumbu TUZ/78/16/2015/2016/VOL.II/6 kutoa taarifa kuhusu
kuwasili kwa karatasi za kupigia kura kwa ajili ya Uchaguzi wa marudio
wa tarehe 20 Machi 2016 na kuitaka CUF kutuma majina mawili ya
watakaoshiriki katika mapokezi ya karatasi hizo.
Bila ya shaka, Tume imo katika mpango wa kuilazimisha na kuishurutisha CUF, hata kama haitaki, kushiriki katika uchaguzi huo kama inavyothibika katika hatua mbalimbali za Tume hiyo ikiwa ni pamoja na kuchapicha majina, nembo na picha za wagombea wa CUF katika karatasi za kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio hata baada ya CUF kukataa kushiriki katika uchaguzi huo
Bila ya shaka, Tume imo katika mpango wa kuilazimisha na kuishurutisha CUF, hata kama haitaki, kushiriki katika uchaguzi huo kama inavyothibika katika hatua mbalimbali za Tume hiyo ikiwa ni pamoja na kuchapicha majina, nembo na picha za wagombea wa CUF katika karatasi za kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio hata baada ya CUF kukataa kushiriki katika uchaguzi huo
Tukiwa
tunakaribia siku ya Uchaguzi wa marudio, CUF imebaini njama kadhaa mpya
zinazoratibiwa na baadhi ya viongozi wa CCM na kutekelezwa na baadhi ya
watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Miongoni
mwa mbinu hizo ni pamoja na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na askari wa vikosi vya Idara Maalum ya
Zanzibar na askari wa majeshi yaliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Polisi na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopo
Zanzibar, ya kuhakikisha wanajitokeza kwa lazima katika uchaguzi wa
marudio na kuipigia kura CCM.
Pia,
kumekuwepo na mpango wa kuandaliwa kwa mawakala ‘feki’. Katika hili
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inashirikiana kwa karibu na kwa kiasi
kikubwa na baadhi ya watendaji wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
wakiwemo viongozi wa vikosi vya idara maalum, kuandaa watu, ambao wengi
wao ni askari wa vikosi hivyo, watakaopewa vitambulisho vinavyowaonesha
kuwa ni mawakala wa CUF, na kutumia majina ya mawakala wa CUF wa 25
Oktoba 2015, na kusambazwa katika maeneo yote ya Uchaguzi nchi nzima.
Lengo
la mpango huu ni kutaka kuwahadaa wanachi kuwa CUF ilishiriki Uchaguzi
kwa kuwa ilitoa mawakala walioshiriki katika Uchaguzi.
Pia,
mpango huu unalenga katika kuzusha hali ya kutofautiana miongoni mwa
uongozi wa CUF na wanachama wa kawaida ili ionekane uongozi wa juu wa
CUF umewasaliti wananchi katika dakika za mwisho kuelekea uchaguzi wa
marudio.
Kwa
upande mwengine, CCM yenyewe imekuwa inaongoza mkakati maalum wa
kuwatafuta baadhi ya waliokuwa mawakala wa CUF katika uchaguzi wa terehe
25 Oktoba 2015, na kuwapa fedha nyingi ili wakubali kuwa mawakala wa
CUF katika uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi 2016.
Ili
kuhakikisha lengo la kuwatumia mawakala hao kufanikisha mchezo wao
mchafu waliouanza mara tu baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa tarehe 25
Oktoba, 2015, CCM imekuwa ikiwazaini mawakala hao wa CUF kwa ahadi
mbalimbali za fedha na vitu vya thamani.
Kutokana na hayo yote tuliyoyaeleza kwa kina, CUF-Chama Cha Wananchi:
Kutokana na hayo yote tuliyoyaeleza kwa kina, CUF-Chama Cha Wananchi:
•
Kinatoa wito kwa wananchi wote kufuata kwa umakini na ukamilifu
maelekezo na kauli za viongozi wazalendo, wanaoitakia mema nchi hii kwa
kuchukua juhudi kubwa kuinusuru na mifarakano ya aina zote, kususia kile
kinachoitwa uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika siku ya
Jumapili, tarehe 20 Machi, 2016 kwa kukaa majumbani mwao kwa utulivu na
kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima ili kujikinga na dhamira na
matendo maovu ya kiharamia yaliyopangwa na kikundi cha wahuni wachache
wa kisiasa dhidi ya raia wasio na hatia.
•
Kinawafahamisha na kuwatanabahisha wafuasi wake na wananchi wengine
wote walioamua kuchagua mabadiliko ya kiuongozi katika nchi yetu katika
uchaguzi uliopita kwamba haijawasilisha jina hata moja la mtu yoyote
kama mapendekezo yake kwa ajili ya mawakla watakaotumika katika uchaguzi
wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016 kwa hivyo haitokuwa na wakala hata
mmoja kwa ngazi yoyote katika uchaguzi wa tarehe 20 Machi, 2016. Ni
muhimu kwa wanachi kuachana na propaganda zilizopitwa na wakati
zinazoenezwa na CCM kuhusu mikakati ya CUF kuelekea 20 Machi, 2016.
•
Mbali na kutoshiriki uchaguzi wa marudio unaosimamiwa na ZEC, pia CUF
inawataka wanachama, wafuasi wake na wananchi wote kutoshiriki katika
uchaguzi wa marudio katika Jimbo la Kijitoupele unaosimamiwa na Tume ya
Tiafa ya Uchaguzi (NEC). CUF inawataka wananchi kususia uchaguzi huo kwa
sababu kwa Zanzibar ni ZEC ndio hufanya kazi kama wakala wa NEC, hivyo
hakuna haki itakayotendeka katika uchaguzi huo.
•
Kinawataka wananchi wote kufahamu kuwa suala la kushiriki uchaguzi ni
suala la mtu binafsi na hakuna mtu au mamlaka yoyote yenye uwezo wa
kulazimisha watu kushiriki katika suala hilo. Chama kinawataka wananchi
kuwa watulivu na kuondoa khofu kutokana na idadi kubwa ya askari wa JWTZ
na Polisi wanaoranda randa mitaani wakiwa na silaha nzito. CUF
inawaomba wananchi kubaki na msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi.
•
Kinawasihi wale wote waliotishwa kwa kunyang’anywa vitambulisho vyao
vya Mzanzibari na vitambulisho vya kupigia kura, kutotishika na hatua
zinazochukuliwa sasa na watendaji waandamizi wa SMZ na mawakala wao kwa
kukataa dhulma na kutumiliwa nguvu katika mambo yaliyo chini ya khiari
zao. Pia, CUF inawasihi wananchi hao kuonesha msimamo wao katika kulinda
na kutetea haki zao za kikatiba na kuonesha mapenzi yao kwa nchi yao
kwa kukataa ukiukwaji wa Katiba na uvunjwaji wa Sheria za nchi yetu kwa
kushiriki katika ukandamizaji na uvizwaji wa demokrasia nchini.
•
Kinawakumbusha askari wa vikosi vyote, walio na uchungu na mapenzi mema
na nchi yetu, kukataa kutumiwa na wanasiasa walioweka mbele maslahi yao
binafsi na kuusahau umma wa wananchi wanyonge wa nchi hii.
Ni vyema kwa askari hawa kutambua kuwa wao ni sehemu ya jamii yetu na kwamba shida na maisha magumu tuliyonayo yanawahusu na kuwakumba kama raia wengine wote. Kukataa kwao kuwa ngazi ya viongozi wanaotafuta hadhi na heshima kwa kupitia migongo ya wengine kutawatoa wao katika idhilali ya kutumika kila nyakati za uchaguzi zinapowadia na kutelekezwa hadi kipindi kama hicho baada ya miaka mitano ambapo hutafutwa na kupewa tena ahadi kemkem zisizotekelezwa.
Ni vyema kwa askari hawa kutambua kuwa wao ni sehemu ya jamii yetu na kwamba shida na maisha magumu tuliyonayo yanawahusu na kuwakumba kama raia wengine wote. Kukataa kwao kuwa ngazi ya viongozi wanaotafuta hadhi na heshima kwa kupitia migongo ya wengine kutawatoa wao katika idhilali ya kutumika kila nyakati za uchaguzi zinapowadia na kutelekezwa hadi kipindi kama hicho baada ya miaka mitano ambapo hutafutwa na kupewa tena ahadi kemkem zisizotekelezwa.
•
Kinamnasihi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John
Pombe Magufuli kutambua kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
lililo chini ya amri yake kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, linaendesha vitisho kwa wananchi kutokana na kuonekana kwa
wingi wakiwa na silaha nzito katika maeneo ya wananchi.
CUF inamtaka Mheshimiwa Magufuli kuondosha majeshi yake yanayoshirikiana na Polisi na vikosi vya SMZ kuendesha unyanyasaji na udhalilishaji wa raia wasio na hatia.
CUF inamtaka Mheshimiwa Magufuli kuondosha majeshi yake yanayoshirikiana na Polisi na vikosi vya SMZ kuendesha unyanyasaji na udhalilishaji wa raia wasio na hatia.
CUF-Chama
cha Wananchi kinawataka wanachama, wafuasi wake na wananchi wote
waliochagua mabadiliko ya uongozi wa kisiasa katika nchi yetu na
kuonesha msimamo wao wa kuikataa CCM kupitia sanduku la kura tarehe 25
Oktoba, 2015 kutovunjika moyo na siasa uchwara zinazoendeshwa na CCM kwa
lengo la kuwatoa katika mstari wa kupigania ushindi wetu mkubwa
tulioupata.
Tunawahakikishia kuwa subra zao na jitihada kubwa inayochukuliwa na Viongozi wa Chama Chetu vitachochea kufikiwa kwa malengo yetu na maamuzi yao ya kuchagua mabadiliko yatazingatiwa na kuheshimiwa.
Tunawahakikishia kuwa subra zao na jitihada kubwa inayochukuliwa na Viongozi wa Chama Chetu vitachochea kufikiwa kwa malengo yetu na maamuzi yao ya kuchagua mabadiliko yatazingatiwa na kuheshimiwa.
NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU-CUF ZANZIBAR
NAIBU KATIBU MKUU-CUF ZANZIBAR
0 comments: