Monday, 17 March 2014

Wasomali wailaani al-Shabaab kwa kutumia watoto kufanya mashambulizi ya kujitoa muhanga

Wazazi nchini Somalia wanaelezea hasira zao kutokana na matumizi ya watoto walio chini ya miaka 18 kwenye mashambulizi ya kujitoa muhanga kulikofanywa na al-Shabaab wakati kundi hilo lilipoendesha mashambulizi yake ya kigaidi mwezi Februari mjini Mogadishu.Baada ya makamando wa al-Shabaab kufanya mashambulizi ya kujitoa muhanga siku ya tarehe 21 Februari dhidi ya jengo la Villa Somalia, viongozi wa al-Shabaab waliwapanga raia kwenye maeneo wanayoyadhibiti kuandamana kuunga mkono kundi hilo la kigaidi.Jioni hiyo, afisa wa ngazi za juu wa al-Shabaab, Fuad Mohamed Qalaf, anayefahamika kama Fuad Shangole, alizungumza na mamia ya raia waliokusanyika kwenye uwanja mmoja wa wazi wilayani Bardhere katika mkoa wa Gedo.Wakaazi hao wanaripotiwa kuamriwa kuhudhuria kwenye hotuba hiyo ya dakika 30 ya Shangole, ambayo ilikusudiwa kuwashawishi wananchi kupambana na wanajeshi wa Ethiopia wanaopanga mashambulizi dhidi ya al-Shabaab kama sehemu ya ujumbe wa Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM)."Kinachotakiwa kutoka kwenu ni kwa Waislamu wote mkoani Gedo kubeba silaha zao," alisema. "Hawa [Waethiopia] wanawauwa watoto wenu, wanaharibu majumba yenu, wanawabaka wasichana wenu na wanachukuwa mali yenu. Hawana uhusiano nanyi kwani [Muethiopia] humuua yule mtu aliye karibu sana naye. Punda na [Waethiopia] hawana huruma."Shangole aliwaamuru watu wa Gedo kufanya mafunzo na wanamgambo hao kwa kile kinachoitwa vita vyao vya jihadi."Ni faradhi kwenu nyote....kubeba silaha zenu na kusafisha bunduki zenu," alisema. "Tutafungua vituo vikubwa na kuwapa watu mafunzo kwa muda mfupi. Wale wanaopewa mafunzo wataungana kwenye mapambano mara moja. Kwa rehema za Mungu Mtukufu, kafiri atapoteza na Ethiopia itashindwa."Siku iliyofuatia, al-Shabaab waliwalazimisha wakaazi wa wilaya ya Bulo Burde mkoani Hiran kuhudhuria kwenye mkutano wa umma ambako waliwaonesha wanawake na watoto wadogo wakiwa wanapunga bunduki zao hewani. Kundi hilo pia lilichapisha kwenye mtandao unaowaunga mkono mkururo wa picha zinazoonesha wanawake na watoto wenye silaha katika jaribio la kuonesha nguvu zake na kujipigia debe.

Itikadi ya al-Shabaab 'haina msingi wa kidini'

Lakini badala ya kuwashawishi watu kubeba silaha zao kwa ajili ya al-Shabaab, Wasomali wengi walielezea fadhaa na hasira zao kwa jinsi ambavyo wapiganaji waliokufa kwa ajili ya kundi walivyokuwa watoto sana.Sahra Yasin, mama wa watoto wanane mwenye umri wa miaka 39 anayeishi wilayani Hamar Weyne mjini Mogadishu, alisema alikerwa sana na picha alizoona kwenye televisheni baada ya mashambulizi dhidi ya jengo la Villa Somalia na wiki moja baadaye kwenyeMkahawa wa Suubiye karibu na makao makuu ya Usalama wa Taifa wa Somalia mjini Mogadishu."Kwangu wote wanaonekana kama vile walikuwa chini ya miaka 18, hasa wale watoto waliotumika kwenye milipuko katika kasri ya rais," aliiambia Sabahi. "Kile al-Shabaab wanachowatumilia watoto wetu hakikubaliki na ninatoa wito kwa wakaazi wote wa Mogadishu kuandamana dhdi ya al-Shabaab kuwatumia watoto kufanya mashambulizi ya kujilipua.""Mimi ni mama. Watoto wanaotumika kufanya mashambulizi ya kujilipua ni kama wanangu," alisema. "Ninaumia vile vile [kama kwamba ni wanangu mwenyewe]."Mkaazi wa wilaya ya Huriwa, Ahmed Ali mwenye umri wa miaka 39, alisema ni jambo la kulaaniwa sana kwamba al-Shabaab inatumia vifo vya watoto wadogo kujijengea jina."Kwa hakika inashitusha sana kwamba al-Shabaab inawafunga milipuko watoto na kuwaambia kuwa watakwenda peponi kwa kujilipua katikati ya raia Waislamu," aliiambia Sabahi. "Hakuna shaka kabisa kwamba lengo la al-Shabaab ni kuhakikisha kuwa wanaonekana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kwa siku mbili za kwanza [baada ya mlipuko huo].""Ninauona mpango wa al-Shabaab kama wa kuwaangamiza watu kwa mauaji ambao hauna msingi kwenye dini," alisema.

Wazazi, serikali lazima wawalinde watoto

Ali, baba wa wavulana wawili, aliwatolea wito wazazi kuwa na hadhari sana na watoto wao na kuvijulisha vyombo vya usalama wakiona ishara zinazoonesha kwamba watoto wao wako kwenye hatari ya kutekeleza itikadi potofu ya al-Shabaab."Mtu yeyote mwenye watoto anaweza kufahamu [kile kinachoumia] kwa al-Shabaab kutumia watoto katika milipuko. Ninawaomba wazazi kuvijulisha vyombo vya usalama wakishuku kuwa watoto wao wanakaribia [kuzungwa] na al-Shabaab," alisema, akiongeza kwamba wazazi wanapaswa kujenga uhusiano wa karibu na watoto wapo ili waweze kufahamu kinachotokea kwenye maisha yao.Sharmarke Ali, baba wa watoto saba mwenye miaka 28 wilayani Hamar, alisema hatua ya al-Shabaab kuwapa mafunzo watoto inaweza kuzuiwa ikiwa serikali itadumisha kampeni yake ya uanzilishaji wa Go 2 School."Haitakuwa na maana [kwa usalama wa Somalia] ikiwa tunasema tu kuhusu namna al-Shabaab inavyowazuga na kuwashawishi watoto kwamba watakwenda peponi ikiwa watajilipua," aliiambia Sabahi. "Kuwaokoa watoto wa Somalia, lazima serikali ije na mpango ambao utawapa watoto wa Somalia fursa ya elimu bure."

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: