Tuesday, 15 April 2014

HABARI HII FEKI IMEWAHADAA WENGI FACEBOOK


Hivi karibuni katika mtandao wa FACEBOOK kumezagaa post inayoeleza uwepo wa VIDEO inayoonyesha NYOKA AKIMLA MAMBA.
Na ukibofya link husika utaaambiwa kwanza SHARE hiyo habari ili uweze kufungua hiyo video.
Na hata uki share hakuna KITU cha ziada. Huo ni UZUSHI tuu.
Kuna watu wanaamua kucheza na AKILI ZAKO ili kukudharirisha kwa kuonyesha kuwa haupo makini. Ipo hivi:-
-- Wewe mwenyewe kabla ya kushare jiulize kama kweli video ipo kwa nini wasiruhusu tuu ionyeshwe mpaka eti wewe ufanye KUSHARE hiyo habari.
---Je, haukuweza ku hakiki taarifa hii kwa kusearch kwa GOOGLE kwa mfano ?
---Kwa nini ukubali kulazimishwa ku SHARE taarifa?
Kuwa makini na taarifa za uongo wa namna hii , wajanja wanaweza kutumia kuingia kwa akaunti yako wakaiba taarifa zako au hata kuamua kupost kwa wall yako kwa niaba yako.
Cheki picha ya post ninayoizungumzia hapa chini kwenye comment.

Niliandika kuhusu habari hii ya NYOKA KUMEZA CHATU, na nilifanya utafiti kwa vyombo vyote vikubwa vya habari hakuna hata kimoja kilichokuwa na VIDEO. Pia isitoshe eneo linalotwaja FRANCH sio sahihi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: