Monday, 28 April 2014

STEVE NYERERE: WASANII FEKI WANAICHAFUA BONGO MUVI

Stori: Mayasa Mariwata
MWENYEKITI wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii feki wana tabia chafu zinazoichafua taasisi hiyo, jambo ambalo hawezi kukubaliana nalo.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akisisitiza jambo.
Akipiga stori na paparazi wetu, kiongozi huyo alisema anashangazwa na wasanii hao wengi wao wakiwa wa kike ambao skendo kwao siyo ishu na wamekuwa wakijitambulisha kama wasanii wa Bongo Muvi.
Stive Nyerere.
“Watu wengi wanapenda kujisema wapo Bongo Movie wakati hawatambuliki kabisa kwenye chama chetu, yote hiyo ni sababu ya kutaka kukuza majina kwa kuwa wanaona umoja huu umeshika chati, lazima nitalito-komeze swala hilo, kama mtu anatamani kuwa mwenzetu ni bora ajiunge akiwa msafi na siyo kutuchafua,” alisema Steve.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: