Saturday, 19 April 2014

UJIO MPYA WA RAY C KATIKA LUNINGA YAKO HABARI ZAIDI TWENDE CLICH HII


Ray C anaendelea na juhudi za kuelimisha jamii katika kupambana na utumiaji wa madawa ya kulevya yanayoharibu kizazi hiki.

Mwimbaji huyo kupitia ‘Ray C Foundation’ ameandaa kipindi maalum kitakachokuwa kinarushwa kwenye TV hivi karibuni.

Kipindi cha Pamoja Inawezekana kinaletwa kwenu na Ray C foundation na kitaanza rushwa kwenye TV zenu hivi karibuni..” ameandika Ray C kwenye Instagram na kuambatanisha picha akiwa na JB.

Job alipokuja kututembelea studio ktk kipindi chetu cha Pamoja inawezekana kitakachorushwa hivi karibuni...kipindi cha Pamoja inawezekana kinaletwa kwenu na Ray C Foundation.” Aliandika katika post nyingine akiwa na JB.

Ray C amejipanga kutimiza sehemu kubwa ya ndoto na ahadi zake baada ya kusaidiwa na rais Kikwete katika matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambapo aliahidi kurudi katika game kama zamani.

Tayari amesharekodi nyimbo kumi katika studio nne tofauti. Muda wowote tutamsikia tena Ray C kama zamani.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: