Shambulizi hili linadaiwa kufanywa na Boko Haram ingawa kundi hilo halijakiri kulitekeleza
Polisi nchini Nigeria wanasema
kuwa shule ya mabweni ya wasichana imeshambuliwa katika jimbo la Borno
Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao.Washambuliaji wanaaminika kuwa wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wanajeshi wawili waliuawa huku mali ikiharibiwa wakati wa shamblizi hilo mjini Chibok.
Mnamo siku ya Jumatatu, zaidi ya watu 70, waliuawa katika milipuko miwili ya mabomu katika kituo cha mabasi mjini Abuja.
Kundi la Boko Haram pia limelaumiwa kwa kufanya shambulizi hilo.
0 comments: