Thursday, 1 May 2014

KIGOGO USALAMA WA TAIFA AUWAWA KINYAMA DAR


Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?
Last edited by Mohamedi Mtoi
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: