Thursday, 22 May 2014

Mbeya City yaenda Sudan


MBEYA CITYTimu ya Mbeya City inaondoka leo usiku kwenda Sudan kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin inayoanza kutimua vumbi kesho Mei 23 jijini Khartoum, Sudan.

Kikosi cha Mbeya City chenye watu 25 wakiwemo wachezaji 20 kinaondoka saa 2.55 usiku kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo kesho (Mei 23 mwaka huu) saa 5 asubuhi kitaunganisha ndege nyingine hadi Khartoum.
Msafara huo wa kikosi hicho ambao utawasili Khartoum saa 7.30 mchana kwa saa za huko unatarajia kurejea nyumbani Juni 5 iwapo timu hiyo itafanikiwa hatua ya mwisho ya mashindano hayo.
Michuano ya Nile Basin imeanzishwa mwaka huu na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), na inashirikisha timu zilizoshika nafasi za pili katika ligi za nchi wanachama wa baraza hilo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: