|
Wema na Kajala |
Ule mgogoro wa mastaa wawili ambao wote ni waigizaji wa filamu nchini
Wema Sepetu na Kajala Masanja umefika kwa waheshimiwa wabunge ambao
wamewataka mastaa hao wawili kukaa chini na kumaliza tofauti zao na kuwa
mashostito wa kutupwa kama awali. Kwa mujibu wa chanzo kimoja makini
kikizungumza na
Globapublishers
wabunge hao ambao wengi wanapenda sanaa wamemwambia kiongozi wa kundi
la Bongo Movie Unity Steve Nyerere afanye juu chini Wema na Kajala
wamalize ugomvi wao na kama akishindwa basi awaambie ili wao wawakalishe
chini kwa kuwa wasanii hao wana majina makubwa na kuna chipukizi wengi
wanawangalia ili kufikia walipo hivyo haileti picha nzuri kwa kuwa huko
mwanzo walikuwa marafiki wazuri na mfano wa kuigwa.
"
Walimwambia
Steve kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana,
hiyo inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha
kushikamana kwa umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya kulumbana" kilisema chanzo hicho.
Nae Steve Nyerere alipotafutwa na GPL alikiri waheshimiwa wabunge kumwambia suala hilo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
0 comments: