KABLA HUJAMWACHA MWENZAKO…SOMA
HAPA
KABLA HUJAMWACHA MWENZAKO...SOMA
HAPA
Miaka 10 ya ndoa yetu siku moja niliingia
nyumbani nikamkuta mke wangu
akiniandalia chakula cha usiku. Nilimshika
mkono na kumwambia: “Nina jambo
ninalotaka kukueleza.” Alikaa na
kunisikiliza kwa makini. Dalili za wasiwasi
nilikuwa nikizishuhudia machoni mwake.
Ghafla nilijikuta katika hali ya kushindwa
kukifungua kinywa changu. Lakini ilikuwa
ni lazima ajue ninachokifikiri a, hivyo
nilipiga moyo konde, nikamwambia kwa
upole: “Ninataka tuachane.” Hakuonekana
kuudhika kwa hoja niliyokuwa
nimeiwasilisha mbele yake, bali aliniuliza
kwa sauti ya upole kabisa: “Kwa nini?”
Nilijaribu kulikwepa hilo swali, hivyo
alighadhibika sana na kuniambia kwa
sauti ya juu: “Wewe si mwanaume!” Usiku
ule hatukusemeshana na muda wote
alikuwa akilia. Nilitambua kuwa alitaka
kujua kitu gani kimetokea katika ndoa
yetu. Lakini sikuweza kumpa jibu lenye
kuridhisha; kwa sababu sikuwa na
mapenzi naye tena, moyo wangu ulikuwa
umetekwa na binti mwingine aitwaye
Jane. Nilimsikitikia sana!
Huku nikiwa na hisia za hatia moyoni
mwangu, niliandika pendekezo la talaka
ambalo lilieleza kuwa atachukua nyumba
yetu, gari na shea ya asilimia 30 ya
kampuni yangu. Mke wangu aliitazama
karatasi hiyo kisha akaichana na kuitupa
kwenye ndoo ya takataka. Huyu ni
mwanamke aliyekuwa ameishi nami kwa
muda wa miaka kumi alikuwa amegeuka
kuwa kama mgeni kwangu. Nilisikitika
sana na kumuomba radhi kwa
kumpotezea muda, rasilimali na nguvu
zake lakini sikuweza kutengua kauli yangu
kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana
Jane na nilikuwa nimezama kweli kweli
ndani ya huba lake na kuwa teja wa penzi
lake. Hatimaye alilia kwa sauti mbele yangu,
jambo ambalo nilikuwa nikitarajia kuliona.
Kilio chake kwangu kilikuwa kama faraja.
Wazo la talaka lililonitawala kwa wiki
kadhaa lilikuwa likizidi kupata nguvu na
sasa lilionekana kuwa wazi kabisa.
Siku iliyofuata nilirudi nyumbani nikiwa
nimechelewa na kumkuta akiandikandika
kitu mezani. Sikutaka kula chochote zaidi
ya kuelekea moja kwa moja kitandani kwa
sababu nilikuwa nimechoka sana
kutokana na mishemishe za siku hiyo
nikiwa na Jane. Niliposhtuka, bado alikuwa
hajatoka mezani. Sikujali hata kidogo,
nikageuka na kuendelea kuuchapa
usingizi.
Asubuhi alinipatia masharti ya talaka:
hakutaka mali yoyote kutoka kwangu, bali
alitaka kuwe na muhula wa mwezi mmoja
kabla ya talaka. Alitaka kwamba katika
kipindi hicho tujaribu kuishi kama
kawaida kwa kadiri iwezekanavyo. Hoja
yake ilikuwa wazi: mtoto wetu alitarajia
kufanya mitihani ya shule ndani ya mwezi
huo na hakutaka tumchanganye kwa tukio
la talaka.
Hili nililikubali. Lakini alikuwa na nyongeza:
alinitaka nikumbuke siku ya ndoa yetu
nilipomnyanyua kumpeleka chumbani
kwetu. Alitaka kwamba katika kipindi
hicho cha mwezi mzima niwe nambeba
kila siku asubuhi kumtoa chumbani mpaka
mbele ya mlango wa nje ya nyumba.
Nilihisi kuwa alikuwa ameshikwa na
wendawazimu. Nilikubali ombi lake kwa
sababu niliona kuwa mwezi mmoja sio
kitu, kwani nilitaka tuachane.
Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya
talaka yaliyotolewa na mke wangu.
Alicheka sana na kuona kuwa ni upuuzi.
“Hata akitumia hila gani lazima apewe
talaka,” alisema Jane kwa masihara. Tangu
nilipoelezea nia yangu ya kutaka kuachana
naye, hatukuwa na uhusiano wa kimwili
na mke wangu. Hivyo nilipombeba siku ya
kwanza, sote tulionekana kutokuwa na
uchangamfu. Mtoto wetu alifurahi na
kupiga makofi: “Baba amembeba mama”.
Kauli yake ilinipa maumivu moyoni. Kutoka
chumbani mpaka barazani, kisha
mlangoni, nilitembea mita kumi nikiwa
nimembeba mikononi mwangu.
Aliyafumba macho yake na kuniambia kwa
upole na ulaini: “Usimwambie mtoto wetu
kama tunaachana.”
Nilikubali kwa kutikisa kichwa huku nikiwa
nimefadhaika. Nilipofika nje nilimshusha
akaenda kituoni kusubiri basi, nami
nikachukua gari langu na kwenda ofisini
nikiwa peke yangu.
Siku ya pili tulijaribu kutoonesha hali
yoyote ya mifarakano. Aliegemea kifuani
kwangu nikahisi manukato mazuri ya
blauzi yake. Nilibaini kuwa sikuwa
nimemtazama vizuri mke wangu kwa
muda mrefu. Uso wake ulikuwa umeanza
kuwa na mikunjo na nywele zake zilikuwa
zimeanza kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa
imemfanya achoke. Kwa dakika kadhaa
niliduwaa na kuwaza kile nilichokuwa
nimemfanyia.
Siku ya nne nilipombeba nilihisi aina ya
ukaribu na mvuto ikirejea. Huyu ni
mwanamke aliyekuwa amenipa miaka
kumi ya uhai na maisha yake.
Siku ya tano na ya sita, kwa mara nyingine,
niliona hali ya ukaribu na mvuto fulani
ikirejea kati yetu. Sikumsimulia Jane
kuhusu hali hii. Kadiri siku zilivyosonga
mbele ndivyo nilivyozidi wepesi wa
kumbeba. Yumkini ilisababishwa na ile hali
ya kumbeba kila siku kiasi cha kumuona
kuwa ni mwepesi.
Asubuhi moja alikuwa akichagua nguo ya
kuvaa. Alijaribu nguo kadhaa lakini
hakupata inayomfaa. Alishusha pumzi na
kusema: “Nguo zangu zote hazinienei,
zimekuwa kubwa”. Nilibaini kuwa alikuwa
amekonda na ndiyo maana niliweza
kumbeba kwa urahisi. Nilisikitika kwa
sababu nilihisi kuwa alikuwa amebeba
mambo mengi moyoni mwake. Hivyo
nilimsogelea na kukipapasa kichwa chake.
Ni wakati huo ambapo mtoto wetu aliingia
na kusema: “Baba sasa ni muda wa
kumbeba mama”. Tukio la kumuona baba
yake akiwa amembeba mama yake
lilimuathiri na kuwa sehemu muhimu sana
ya maisha yake. Mke wangu alimuita na
kumkumbatia kwa upendo. Niligeuza uso
wangu pembeni, sikutaka kuangalia tukio
hilo nisinje nikabadilisha uamuzi wangu
wa talaka. Nilimnyanyua na kumbeba mke
wangu, nikatembea kutoka chumbani,
sebuleni mpaka nje. Aliizungusha mikono
yake mizuri shingoni kwangu, nami
nikamshikilia vizuri; ilikuwa kana kwamba
ni siku ile ya harusi yetu. Lakini wepesi wa
mwili wake ulinifanya niwe mwenye
huzuni.
Siku ya mwisho nilipombeba niliingiwa na
uzito wa kupiga hatua. Wakati huo mtoto
wetu tayari alikuwa shule. Nilimshikilia
vizuri na kusema: “Sikuwa nimejua kuwa
maisha yetu yamekosa mvuto”. Niliwasha
gari kuelekea ofisini, niliamua kupita kwa
Jane. Nilipofika nilitoka haraka bila hata
kuubana mlango wa gari. Nilikuwa na
wasiwasi nisije nikaghairi nia yangu…
nikapandisha ngazi. Jane alipofungua
mlango nilimwambia: “Samahani Jane,
sitaki kuachana na mke wangu”.
Alinitazama kwa mshtuko na kunigusa
kwenye paji la uso. “Una homa?” alisema.
Niliutoa mkono wake na kumwambia:
“Samahani Jane, sitaki kumuacha mke
wangu. Yawezekana maisha yangu na mke
wangu yalikosa uchangamfu kwa sababu
hatukuwa karibu, sio kwa sababu
hatukupendana. Sasa nimebaini kwamba
kwa kuwa nilimbeba siku ya ndoa yetu,
ninapaswa kuendelea kufanya hivyo
mpaka kifo kitutengenishe. ” Jane
alionekana kushtuka sana. Alinizaba kibao,
akaubamiza mlango na kuanza kulia.
Nilimuacha nikapanda gari na kuondoka.
Njiani nilipita kwenye duka la maua
nikaagiza shada la maua kwa ajili ya mke
wangu. Muuzaji akaniuliza ujumbe
unaotakiwa kuandikwa juu ya kadi
nikatabasamu na kumwambia aandike:
“Kila siku asubuhi nitakubeba mpaka kifo
kitakapotutenga nisha”.
Jioni nilifika nyumbani nikiwa na maua
mkononi, tabasamu usoni, nikapandisha
ngazi mpaka ndani. Nilipofika chumbani
mke wangu alikuwa amelala akiwa
amefariki dunia. Kumbe alikuwa
akipambana na KANSA kwa miezi kadhaa
lakini sikujua kwa sababu nilikuwa
nimetekwa na Jane. Bila mimi kufahamu,
kumbe marehemu mke wangu alijua
kwamba muda si mrefu atafariki dunia na
alitaka kuniokoa dhidi ya fikra yoyote
mbaya kutoka kwa mtoto wetu kama
tungeachana muda mfupi kabla ya kifo
chake. Angalau machoni mwa mwanangu
naonekana kuwa mume mwenye
upendo…
WAPENDANAO NATAKA MJIFUNZE
1) Wengi wanatengana si kwa sababu
hawapendani, bali hawapeani muda wa
kusikilizana.
2)Wengi wanaamini ukiachana na
mpendwa wako ni lazima muwe maadui.
3)Busara ndani ya pendo ni zaidi ya mali
na pesa.
4)watanzania tupo 44 milioni.. wanawake
ni 24 milioni na wanaume 19 na ushee..
hivyo kama kila mwanaume ataoa mke
mmoja basi kuna wanawake milioni 5 kazi
yao itakuwa kuvizia waume za watu. abiria
chunga mzigo wako atiiii.
BONGE LA STORI ILA KAMA UNAROHO NYEPESI USISOME UTALIA BURE NDUGU
published on 13:14:00
leave a reply
0 comments: