Wednesday, 11 June 2014

Jennifer Lopez kutumbuiza katika ufunguzi Kombe La Dunia Brazil kesho

Ufunguzi rasmi wa fainali za kombe la dunia nchini Brazil unatarajiwa kufanyika kesho Alhamisi (June 12), Jennifer Lopez anatarajiwa kuungana na rapper Pitbull pamoja na Claudia Leitte kutumbuiza wimbo rasmi wa kombe la dunia katika sherehe hizo.Pamoja na FIFA mapema wiki hii kutangaza kuwa Lopez asingetumbuiza katika ufunguzi huo, muwakilishi wake amethibitisha uwepo wake kwa PEOPLE, kwa mujibu wa Aceshowbiz. “Jennifer has always wanted to participate in the World Cup opening ceremonies, we have been trying to work out scheduling and logistics. Any statements to the contrary were premature. Jennifer would not want to disappoint her fans or fans of futbol. She will be there.” Alisema muwakilishili huyo. J’Lo rapper Pitbull na muimbaji wa Brazil Claudia Leitte wameshirikiana katika wimbo rasmi wa kombe la dunia mwaka huu uitwao ‘We Are One (Ole Ola)’.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: