Monday, 9 June 2014

Kenya wazuia magari na wakala wa utalii TZ kuingia mbuga za wanyama

Baadhi ya watalii wakitumia vivutia picha kuangalia wanyama kwenye moja ya mbuga za wanyama nchini Tanzania. Serikali ya Kenya imewazuia waendeshaji wa utalii na magari ya Tanzania kupeleka watalii nchini Kenya.
Baadhi ya watalii wakitumia vivutia picha kuangalia wanyama kwenye moja ya mbuga za wanyama nchini Tanzania. Serikali ya Kenya imewazuia wakala wa utalii na magari ya Tanzania kupeleka watalii nchini Kenya.
Mamlaka ya Udhibiti wa Utalii nchini Kenya (Kenya’s Tourism Regulatory Authority) imewazuia wakala wa utalii na magari wa Tanzania kuchukua watalii na kuwapeleka kwenye mbuga za Kenya.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la Kenya, hatua hiyo ya TRA n majibu sawa na kitendo cha mamlaka ya utalii Tanzania, ambao wanashutumiwa kwa kuwafungia makusudi waendeshaji utalii wa Kenya kuingia kwenye mbuga za Tanzania.
Hata hivyo, Mamlaka ya Mbuga za Wanyama Tanzania (TANAPA) iliiambia gazeti la The Citizen kuwa hatua hiyo inaendana na sheria Tanzania zinazodai kuwa huduma hiyo inapaswa kutolewa ndani ya mipaka ya kila nchi husika.
Kiongozi wa TRA Korir Lagat, wakati akizungumza na washika dau wa utalii alisema “sula hilo limekuwa la kawaida na Kenya haitoweza kurudi nyuma.
Kutokana na barua iliyotumwa Huduma ya Wanyamapori Kenya inaeleza ni kwamba magari yote yenye nambari za usajili za Tanzania hayataruhusiwa kuingia kwenye mbuga za wanyama.”
Naye Afisa Uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete alisema, sio kweli kwamba kila gari lenye nambari za usajili za Kenya limekuwa likisumbuliwa au kukataliwa kuingia kwenye mbuga za taifa.
“Familia ya Kenya zilizo na magari yao binafsi zinakaribishwa muda wowote wanaotaka kuingia kwenye mbuga za wanyama.”
Shelutete alisema, uzuiaji, “upo kwa wakala wa utalii na magari yao yaliyosajiliwa”, hayo ndio makubaliano baina ya nchi hizi mbili tangu mwaka 1985.
Chanzo: Mwananchi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: