Friday, 17 October 2014

ROSE MUHANDO AANDAMWA KWA TUHUMA ZA UTAPELI

   
Mhando
Na Andrew Carlos wa Global Publishers
MWANAMUZIKI mkali wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amedaiwa tena kuhusika katika utapeli wa shilingi milioni mbili.

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Rose Muhando.
Muandaaji wa shoo hiyo, Ibrahim alidai kuwa Rose alitumiwa kiasi hicho cha pesa kama sehemu ya malipo ya kazi hiyo iliyokuwa ifanyike Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Landmark uliopo Ubungo, jijini Dar lakini hakutokea.
“Huu ni utapeli wa hali ya juu, maana alipewa pesa yote ya shoo, cha kushangaza hakutoa taarifa yoyote ya dharura, simu akipigiwa hapokei na wala meseji hajibu,” alisema Ibrahim.
Rose alipopigiwa simu ili kujua madai hayo kama yana ukweli, simu yake iliita bila ya kupokelewa hivyo akatumiwa meseji ambayo nayo ilionesha kumfikia lakini hakujibu chochote.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu.
Hivi karibuni, Rose alidaiwa kuingia mitini na shilingi milioni moja aliyopewa kama malipo ya kutumbuiza katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, John Lisu
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: