March 15 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
aliwaapisha Wakuu wa Mikoa wapya huku akitoa siku 15 kwa Wakuu wa Mikoa
wawe wamesimamia na kuondoa watumishi hewa na pia kuwakamata vijana
wote ambao hawataki kufanya kazi kwa kuwapeleka katika kambi maalum ili
wakalime.
Leo March 16 2016 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amekutana
na Wakuu hao wa Mikoa na kuwapa mikakati na miongozo ya kiutendaji
katika majukumu yao mapya hasa katika kuchukua hatua kwa watendaji
wazembe mikoani.
Pia amesisitiza kuwabana wao wakuu wa Mikoa kama hawatasimamia vyema majukumu yao, Simbachawene amesema……>>> ‘Mimi
nitashughulika na ninyi, mimi Waziri hapa eti natoka kule naruka
sarakasi kwenye shule ya msingi eti nakagua pale eti darasa limekaa
hivi, mimi nakula na wewe, ukiona nimefika kule ujue una hali mbaya na
sitapita ofisini kwako, mimi nikienda nikikuta shule imeezuliwa
wanafunzi wanasomea chini ya mti najua hakuna Mkuu wa Mkoa hapa’:-George Simbachawene
Aidha waziri huyo amesisitiza Wakuu wa Mikoa kuwasimamia wananchi kufanya kazi…….>>>’ninyi
ndio mnatakiwa kuona kwamba watumishi wote wa umma wanafanya kazi yao
kwa mifumo mtakayoiweka, lakini pia kuhakikisha wananchi kwa ujumla
wanafanya kazi na wakati mwingine mtu unafikiria bora turudishe sheria
ya nguvu kazi ili kila mmoja ajulikane anafanya nini’:-George Simbachawene
0 comments: