Saa chache kabla ya kutangwa kuteuliwa na Rais Rais John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Leo march 13 2016 Paul Makonda akiwa
bado ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliadhimisha mwaka mmoja tangu
kuteuliwa kwake kuiongoza Wilaya hiyo, lakini jambo zuri zaidi
alilolifanya katika siku hii ni pamoja na kuzindua jiwe la msingi la
ujenzi wa jengo la upasuaji, wagonjwa mahututi na mapumziko katika
hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam.
Makonda anasema>>’Leo nimetimiza mwaka mmoja tangu kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, kwangu ni faraja kutimiza mwaka mmoja‘
‘Wakati
nafanya ziara zangu na kuona Mheshimiwa Rais ameenda kutembelea
Muhimbili na kukuta wagonjwa wengi, sisi kama wasaidizi wake ni lazima
tuangalie cha kufanya kwenye maeneo yetu ikiwa ni pamoja na kuangalia
namna ya kuwapunguzwa wagonjwa kutoka muhimbili na kutibiwa katika
hospitali zetu kama Mwananyamala‘ ;-Paul Makonda
‘Baada
ya hilo nikaoona niwatafute wadau ili tusaidiane kujenga jengo la
upasuaji katika hospitali ya Mwananyamala, Wadau wakakubaliana na mimi
na tayari tumeshaanza mchakato wa ujenzi ambao utaanza kesho‘ ;-Paul Makonda
0 comments: